1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KOMBE LA KLABU BINGWA AFRIKA

Na Ramadhan Ali21 Machi 2005

SCHLAKE YAREJESHA USUKANI WA BUNDESLIGA MIKONONI MWA BAYERN MUNICH

KOMBE LA KLABU BINGWA BARANI AFRIKA

NA KENENESA BEKELE AWIKA TENA KATIKA MBIO ZA NYIKA ULIMWENGUNI.

Tukianza na Bundesliga-Ligi ya Ujerumani-Schalke 04,jana imeurejesha usukani wa Ligi mikononi mwa mabingwa mara kadhaa Bayern Munich wakibainisha hawakupevuka kutwaa ubingwa.Schalke iliotarajiwa kuilaza klabu chipukizi ya Mainz ili kuongoza Ligi wazi,ilizabwa mabao 2:1 na hivyo imerudia pale pale ilipokuwapo jumamosi ilipotangulia ilipoizaba Munich bao 1:0.

Mbrazil Lincoln aliipatia schalke bao la mkwaju wa penalty na kufanya matokeo sare 1:1

Matokeo hayo yameifanya Bayern Munich viongozi wa Ligi kufuatia ushindi wao jumamosi wa mabao 3:1 nyumbani dhidi ya Hansa Rostock.Mapambano 8 yakisalia kabla kumalizika msimu, kila moja Bayern Munich na schalke zina point 53 huku Munich ikiongoza kwa magoli.

Stuttgart imesonga mbele nafasi ya tatu ikiwa na pointi 48 kufuatia ushindi wao nyumbani wa bao 1:0 dhidi ya Freiburg.Mabingwa werder Bremen wameangukia nafasi ya 4 baada ya ushindi wao wa mabao 2:1 dhidi ya Nuremberg.

Katika Premier League-Ligi ya uingereza klabu zote 3 za usoni ziliwika mwishoni mwa wiki:Hii ina maana Chelsea itakayokumbana na Bayern Munich katika champions-league-kombe la klabu bingwa barani ulaya,ina nafasi ya kutawazwa mabingwa kwa mara ya kwanza tangu 1955.

Nchini Spain, FC Barcelona inaongoza orodha ya Ligi kwa pointi 11 baada ya kuizaba Deportivo la Coruna bao 1:0.

Olympique Lyon inaendelea kutamba katika Ligi ya Ufaransa ikiania taji lake 4 mfululizo.Lyon iliitandika Strasbourg bao 1.

KATIKA KINYAN’GANYIRO CHA KOMBE LA KLABU BINGWA BARANI AFRIKA:

Kura imepigwa kwa duru ya tatu:mabingwa Enyimba wa Nigeria waliozaba Simba ya tanzania mabao 4:0 huko Aba, watakutana na Red Arrows ya Zambia; etoile du sahel ya tunisia ina miadi na Royal armed Forces ya Morocco.AS Aviacao ya Angola itaikaribisha Zamalek ya Misri wakati Kaiser Chief ya Afrika kusini itaitembelea Esperence ya Tunisia.

Mjini Casablanca, Motema Pembe ya J.K.Kongo ilizabwa mabao 2:0 na Raja Casablanca.Royal Armedr Forces iliikumta Asante kotoko ya Ghana 2:0. Esperence iliitoa Al hilal ya sudan kwa mabao 5:1

Al Ahli ya Misri ilizaba Villa ya Uganda 6:0.

RIADHA:

Katika mbio za ubingwa wa nyika duniani, Muetjiopia Kenenisa Bekele alinyakua jana ushindi wake 4 mfululizo wa mbio hizo huko St.Etienne,Ufaransa.Alishinda mbio hizo za km 12 kwa muda wa dakika 35 na sek.6.

Kenenisa alitimka mbio katika duru ya 5 kati ya 6 na kumuacha nyuma tumaini la Kenya,Eluid Kipchoge.Ushindi wa Kenenisa Bekele uliwatia shime waethiopia kunyakua pia taji la timu tena kwa mwaka 2 mfululizo kufuatia kukomesha enzi ya miaka 18 ya wakenya mjini Brussels mwaka jana.

Mueritrea Zersenay Tadesse alikuja wapili sekunde 14 nyuma ya Bekele huku Abdullah Ahmad hassan wa Qatar-zamani mkenya akija 3.

Ama Upande wa wanawake, Muethiopia Turunesh Dibaba ameshinda mbio za nyika za wanawake n a hivyo kuhakikisha Ethiopia imetwaa mataji yote.Msichana huyu mwenye umri wa miaka 19 alimshinda mwenzake wa Ethiopia Werkenesh Kidane aliemaliza wapili.Waethiopia na wakenya walichukua nafasi 6 za kwanza.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW