1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KOMBE LA KLABU BINGWA AFRIKA

23 Septemba 2005

Tukianza na Bundesliga-Ligi ya Ujerumani,Bayern Munich-mabingwa waliendelea kati ya wiki kutamba kileleni na hawakushindwa hata mara moja tangu kuanza msimu huu.Wakati wakisherehekea rekodi ya kutoshindwa mapambano 15 mfululizo ,timu zilizosalia zinajiuliza iwapo Munich inatoroka na taji la ubingwa na mapema au vipi:jibu linatolewa jumamosi hii Munich ikipambana na Hamburg na ikiongoza orodha ya Bundesliga kwa pointi 4.

Munich inafuatwa nafasi ya pili na Hamburg na ikicheza nyumbani wakati huu, Hamburg imeazimia kutoiwachia munich kuondoka na pointi 3 nyengine na kupanua zaidi mwanya huo wa piointi 4 na kuwa 7.Munich imerudi uwanjani lakini na nahodha wa timu ya taifa aliekua ameumia Michael Ballack na anahitajika sana leo kwavile,Hamburg iliahidi kutoa changamoto kali kwa mabingwa.Wao na Werder bremem ni timu mbili pekee zinazotumainiwa na klabu nyengine kulizuwia taji la msimu huu unaotangulia kombe lijalo la dunia, kubakia Munich.

Mpambano mwengine wa kusisimua jumamosi jioni ni kati ya Werder Bremen inayosimama nafasi ya tatu katika ngazi ya Ligi na Bayer Leverkusen ilioitimua FC Cologne jumatano kwa mabao 2:1.Leverkusen baada ya kumtimua kocha wake Klaus Augenthaler, kocha wa zamani wa timu ya taifa Rudi Völler,amerudi kushika usukani akidai ni kwa muda tu hadi kocha mpya ameteuliwa-nae anatazamiwa kuwa Mathias sommer,aliekuwa kocha wa Stuttgart.Völler tayari ameshinda mapambano 2 tangu ashike usukani na akitamba leo tena mbele ya Bremen-nyumbani mwa Bremen alikokua akicheza zamani, basi vilio vitasikika abakie kocha wa Leverkusen.

Armenia Bielefeld ina miadi na Borussia Mönchengladbach wakati Mainz inacheza nyumbani na Borussia Dortmund.Duisburg inakutana wakati huu na Nuremberg wakati schalke ilioteleza sana nyuma inapimana nguvu na Hannover.Kesho jumapili, duru hii itakamilishwa kwa changamoto 2-FC Cologne ikicheza nyumbani itaikaribisha Hertha Berlin.

Katika kinyan’ganyiro chake na Bayern Munich kumania staid wake Lukas podolski, Cologne imetangaza itayri kumpandishia mshahara na marupurupu Podolski hadi Euro milöioni 2 kwa mwaka.Ikiwa hii itatosha kumtia shime Podolski na kumbakisha cologne,tutaona baada ya firimbi ya mwisho hapo kesho.Mpambano mwengine ni kati ya Stuttgart na Kaiserslauten.

KATIKA LIGI YA UINGEREZA-PREMIER LEAGUE:

Manchester United haina nafasi ya kutwaa ubingwa msimu huu ikiwa itashindwa kuwika katika mapambano 2 kati yake na Blackburn Rovers na Fulham-hii ni kwa muujibu wa staid wao Paul Scholes.Manchester iko pointi 7 nyuma ya mabingwa na viongozi wa ligi-Chelsea.

Arsenal nayo inahitaji kujiwinda zaidi ikiwa nao wanataka kuizuwia Chelsea isitorke na taji na mapema.Arsenal jumamosi ina miadi na West Ham.

Katika Ligi ya Spain, Real Madrid ingali inaregarega msimu huu na mapambano 3 sasa haikuwika.ikicheza bila ya jogoo lao lililoumia Zinedine Zidane ,Real imeshindwa mechi 2 katika La Liga-Ligi ya Spain na moja katika Champions League-Kombe la klabu bingwa barani Ulaya.Pigo jengine, laweza likaongoza kutimuliwa kwa kocha wao mbrazil Wanderly Luxemburgo.

AMA KATIKA NUSU-FINALI 2 ZA KOMBE LA KLABU BINGWA BARANI AFRIKA:

Timu 4 za Afrika ya kaskazini zinaania mwishoni mwa wiki hii tiketi zao za kucheza finali ya Kombe hilo na baadae kuwakilisha bara la afrika katika Kombe la dunia la klabu bingwa huko Japan.

Katika nusu-finali ya kwanza klabu 2 za Misri zitaumana kesho-Zamalek na Al Ahly.

Al Ahly inatetea kesho rekodi yake ya kutoshindwa mechi 44.Mashetani wekundu wa jiji la Cairo hawakushindwa nyumbani tangu walipopata pigo la mwisho na Arab contractors, Juni mwaka jana.Rekodi hii ya ajabu inaifanya Al Ahly kupigiwa upatu kushinda kesho dhidi ya zamalek.Bingwa wa Kombe hili ameahidiwa kitita cha dala milioni 3.5 na ndie atakaewakilisha Afrika katika Kombe la klabu bingwa la dunia hapo desemba nchini japan.

Zamalek illeo na Raja Casablanca ya Morocco.

Mshindi atakutana oktoba ama na Raja au na Etoile du Sahel.Etoile ilitimua Green Devils katika changamoto za mikwaju ya penalty.Jumamosi basi ina miadi na Raja katika uwanja wenye kusheheni hadi mashabiki 80.000 wa mfalme Mohammed V.

Kati ya wiki hii,ndege iliokodiwa na rais wa Gambia kuwasafirisha mashabiki 289 hadi Peru kwa finali ya Kombe la vijana la dunia chini ya umri wa miaka 17, ilitua katika uwanja usioruhusiwa na rubani kujigamba ilipungukiwa na mafuta.Hatahivyo, ndege hiyo ilitua kwa wakati kuiwezesha timu ya Gambia kucheza mpambano wao dhidi ya Qatar.

Kutua huko kwa dharura na bila kutazamiwa kwas ndege hiyo, kulizusha wasi wasi na hali ya hatari mjini Piura,mji wa mwambao wa pwani.Magari ya wazimamoto yakwasili uwanja wa ndege na polisi wakakimbilia huko na mahospitali yakatakiwa yakae tayari kupokea majeruhi.

Mwishoe, mashabiki hao 289 waliingia katika hoteli 5 mbali mbali za mji huo mdogo lakini ndege hiyo waliosafiria ilitiwa nguvuni na wakuu.

Finali ya Kombe hili linalojumuisha timu 16 za dunia itakua Oktoba 2. Ndege hiyo ikitokea Brazil na asili yake ilikua itue mji mkuu Lima.

NJE YA DIMBA:

Katika ringi ya mabondia kati ya wiki hii mbondia maarufu bingwa wa zamani wa taji la shirika la International Boxino Federation wa wezani hafifu-lightweight-Leavander Johnson alifariki hospitali juzi alhamisi.Hii ni siku 5 tangu kupatwa na majaraha makubwa katika ubongo wakati wa ndondi.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW