KOMBE LA KLABU BINGWA AFRIKA
7 Machi 2005BUNDESLIGA-BAYERN MUNICH NA SCHALKE BEGA KWA BEGA KILELENI
-KOMBE LA KLABU BINGWA BARANI AFRIKA
MKENYA JOSEPH RIRI ASHINDA MBIO ZA MARATHON HUKO JAPAN
NA MICHAEL SCHUMACHER AONYA BADO SIKU ZAKE HAZIJESHA
Tukianza na Bundesliga inayojiwinda kwa changamoto za keshoza Champüions League-Kombe la klabu bingwa barani Ulaya kati ya Bayern Munich na Arsenal London,yadhihirika sasa ni mbio za farasi 2:Munich na Schalke ambazo kila moja ina pointi sawa kileleni mwa ngazi ya Ligi:
Michael Ballack jumamosi alivunja ubishi wa mabingwa watetezi-Werder Bremen na kuipatia Munich ushindi wa bao 1:0 na hivyo imesalia kileleni mwa ngazi ya ligi.Bayern Munich inaongoza Ligi kwa wingi wa magoli.
Schalke 04 ilimuona mshambulizi wao wa Brazil-Ailton akitia bao lake la 1000 katika Bundesliga kabla mwananchi mwenzake kutoka Brazil-Lincoln kutia bao la 2 la schalke dhidi ya Bochum.
Hertha Berlin jana ilirudi nyuma katika kinyan’ganyiro cha Kombe la Ligi kufuatia kutoka suluhu tu bao 1:1 na Kaiserslauten.
Werder Bremen –mabingwa wameangukia sasa nafasi ya tatu –pointi 7 nyuma ya Munich na schalke.Hivyo,wanaelekea watavuliwa taji msimu huu.
Kura imepigwa ya nusu-finali ya Kombe la shirikisho la dimba la Ujerumani:
Mabingwa wa Kombe hilo-Bremen watakutana na Schalke wakati Bayern Munich wana miadi na Armenia Bielelfeld.Munich ilizabwa mabao 3:1 na Bielefeld-shukurani kwa mabao ya muafrika Kusini, Delron Buckley.Inavuma Stuttgart inamrandia Buckley kumfungisha mkataba msimu ujao.
KOMBE LA KLABU BINGWA BARANI AFRIKA:
Katika duru ya pili ya Kombe la klabu bingwa barani Afrika,Asante kotoko ya ghana ilitandika FAR Rabat ya morocco bao 1:0.Tusker ya Kenya ililazwa kwa bao 1:0 na Zamalek ya Misri wakati mjini Mwanza, Simba ya Tanzania iliwazima mabingwa Enyimba wa Nigeria sare bao 1:1.
Katika kombe la klabu bingwa, Darling Motema Pembe ya Jamhuri ya kidemokrasi ya Kongo ilimudu suluhu tu na Raja Casablanca ya Morocco mjini Kinshasa.Nimobouna anajishughulisha lakini n a hatima ya Simba wa kongo katika Kombe lijalo la dunia:
RIADHA:
Mkenya Joseph Riri alizima vishindo vya dakika ya mwiasho na kunyakua ushindi wa mbio za maratrhon za Lake Biwa nchini japan hapo jana.Alimshinda chupuchupu bingwa wa mbio hizo Jose Rios.
Riri kwanza aliukosera mlango wa kuingia Uwanja wa Otsu huku adui yake akiwa dakika 15 nyuma.Lakini alirudi nyuma haraka na kutia kasi kuzima vishindo vya hasimu yake kwa muda wa masaa 2: 9:03.
Katika mbio za magari za kwanza msimu huu huko Melbourne,Australia: bingwa wa dunia Michael Schum,acher alishindwa jana kumalioza mbio hizo.Hatahivyo, Schumacher amewaonya maadui zake wasimtoe maanani kwamba mwaka huu hana lake jambo.Bingwa huyu mara 7 wa Grand Prix alianza vibaya sana mbio zake msimu huu na baada ya duru 15 alitoka mashindanoni baada ya kujigonga na dereva Nick Heidfield.