1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kombe la klabu bingwa Afrika

Ramadhan Ali11 Septemba 2006

katika kinyan'ganyiro cha Kombe la klabu bingwa barani afrika Asec Abijan imeilaza jana Orlando Pirates ya Afrika Kusini.Katika mbio za magari,Michael Schumacher kustaafu mwishoni mwa msimu huu.

M.Schumacher kuaga mbio za magari
M.Schumacher kuaga mbio za magariPicha: AP

Klabu 2 za daraja ya kwanza ya Bundesliga-Ligi ya Ujerumani-Mainz na Armenia Bielefeld zilifunzwa darsa la dimba jana na timu za daraja ya 3 na kutimuliwa nje ya Kombe la shirikisho la kabzmbu la Ujerumani (DFB Pokale).

Mainz ilizabwa bao 1:0 na Saarbruecken na bao la dakika ya mwisho la Bielefeld halitosha kuzuwia kuzama kwa mabao 2:1 ya timu chipukizi ya daraja ya tatu SC Pfullendorf.

Lakini si timu hizo mbili pekee zilizoaga na mapema Kombe hili, bali zimejiunga tu na safu nyengine ya timu za daraja ya kwanza kama makamo-bingwa Bremen,Hamburg na Energie Cottbus zilizotimuliwa tayari jumamosi.

Kwa upande mwengine, Hertha Berlin ilitokwa na jasho kabla kuitimua nje timu ya daraja ya tatu ya Darmstadt kwa bao 1:0.Bayer Leverkusen nusra ikione kilichomtoa kanga manyoya,kwani ilibanwa mabao 2:2 na ni kupitia changamoto tu ya mikwaju ya penalty, ndipo Leverkusen ilipookoa na kuizoa Koblenz.

Hata mabingwa wa kombe hili-Bayern Munich walihitaji muda wa kurefushwa kabla kuitimua St.Pauli inayocheza daraja ya 3 kwa mabao 2:1.

Katika Ligi ya Spain, Ruud van Nistelrooy,alitia mabao 3 kuipatia ushindi klabu yake mpya ya Real Madrid kwa mabao 4:1 dhidi ya Levante.

Aliekua nahodha wa Ufaransa hadi kombe lililopita la dunia-Zinedine Zedane,,amesema kwamba amekipa kisogo kisa cha kumpiga dafurau Marco Paterazzi wakati wa finali ya kombe la dunia kati ya Ufaransa na Itali.Zidane, aliestaafu kutoka timu ya Ufaransa mara tu kumalizika Kombe la dunia, alisema alifurahishwa kuiona Ufaraynsa majzi ikiilaza Itali kwa mabao 3:1.

Mtaliana Marco Materazzi aliungama wiki iliopita kwamba alimtukania Zidane, dada yake.

Tukigeukia dimba barani Afrika:

Asec Abidjan ya Ivory Coast imeichezesha jana Orlando Pirates ya Afrika Kusini, kindumbwe-ndumbwe ilipoizaba mabao 4:0 mjini Abidjan.Hii imeihakikisha ASEC nafasi ya usoni kabisa katika kundi hili B pamoja na tiketi ya kucheza nusu-finali ya Champions League-kombe la klabu bingwa barani Afrika.

Pirates ilibidi kucheza dakika 30 na wachezaji 10 tu uwanjani baada ya Jabu Pule kutimuliwa na rifu nje ya uwanja kwa kuchzezea ngware.

Enyimba ya Nigeria ilioilaza Hearts of oak ya ghana bao 1-0 katika changamoto za kundi B mjini Aba mapema jana ,haimudu tena kuipiku ASEC kileleni .Prlando Pirates sasa imeteleza hadi nafasi ya tatu lakini yaweza bado kukata tiketi ya nusu-finali ikimudu kutamba mbele ya Enyimba katika mechi yao ya mwisho mjini Johannesberg,jumamosi hii ijayo.

Esperence ya Tunisia imeionea Renacimiento ya Guinea ya Ekweta - mabao 5:0 katika kombe la Shirikisho la dimba la Afrika.sasa esperence inaitia shindo Etoile Sahel pia ya tunisia inayoongoza kundi B.Etoile iliikumta St Eloi Lupopo yxa H.K.Kongo mabao 4:1.

Nazo timu 2 za morocco zimetamba dhidi ya 2 za angola: Royal Armed Forces imeshika uongozi wa kundi baada ya kuizaba InterClube wakati Olympique Khouribga imechapa Petro Atletco bao 1:0 hapo jana.

MBIO ZA MAGARI:

Mashindano ya mbio za motokaa za formula one-jana yalioonesha heshima yake kwa bingwa wa mabingwa-Michael Schumacher wa Ujerumani, alieshinda jana mbio za ‘Italian Grand Prix’ huko Monza na baadae kutangaza atastaafu baada ya mashindano 2 yajayo.”

Ikiwa bingwa wa mabingwa ulimwenguni anastaafu,bila shaka ni siku ya kuhuzunisha.”-alisema Muastria-bingwa wa zamani Niki Lauda, alieshinda mbio hizi mara 3.

Akaongeza, “Unaweza kusema utakavyo, lakiniSchumacher ameshinda mara saba ubingwa wa dunia na yamkini akashinda tena mara ya mjwisho.Hakuna mwengine kama yeye duniani ,kwani yeye ni wa aina ya kipekee.Inahuzunisha kwamba anastaafu,lakini siku moja inabidi kustaafu na ninaheshimu hivyo.”

Akiwa na umri wa miaka 37,Michael schumacher ameshindana mbio 247 za Formula One na 178 ya mbio hizo kwa magari ya Ferrari.

Schumacher ameshinda mbio 90 mbali mbali, 71 kwa niaba ya Ferrari na amechukua mara 68 nafasi ya kuanza mbio hizo usoni kabisa-Pole positions.

Mwishoni mwa msimu huu, Schumacher atakuwa ameshiriki mbio 250 na hivyo 6 tu kasoro kuliko rekodi ya mtaliana Riccardo Patrese.

Kufuatia ushindi wa jana humo Monza, ameupunguza mwanya wake kutoka dereva wa usoni kabisa msimu huu mspain Fernando Alonso hadi pointi 2.Sasa Michael schumacher, ana kila nafasi ya kun’gatuka akitia mfukoni taji la 8 la ubingwa wa dunia.

Schumacher alinukuliwa baada ya ushindi wake huo jana kusema:

“Imekuwa ikivumishwa sana juu ya siku zangu za usoni.Kwani, inafika siku mtu anabidi kustaafu na kwangu mimi hii ni mwisho wa m waka huu na hivyo natumai pamoja na Ferrari kumaliza kwa kunyakua taji la ushindi.”

Taji la dunia kufuatia ushindi wa jana huko Monza linanyemelea nami nitakua nikilikodolea macho kulitwaa katika mashindano matatu yajayo ili kumaliza kwa ushindi.”-alisema schumacher.

Stadi mwengine alietamba mwishoni mwa wiki,. Ni mswisi Roger Federer katika medani ya Tennis. Federer alinyakua jana taji lake la 3 mfululizo la ‘US OPEN’ baada ya kumtoa Andy Roddick kwa seti 4-6-2,4-6,7-5 na 6-1.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW