Kombe la klabu bingwa barani Afrika
28 Agosti 2006
Katika Bundesliga-Ligi ya Ujerumani,tangu mabingwa BAYERN MUNICH HATA MAKAMO-BINGWA WEDER BREMEN, waliteleza na kupoteza pointi.
Bremen –mabingwa 2004 walishinda mechi zao 2 za kwanza msimu huu mpya sawa na mabingwa Bayern Munich.Mwishonio mwa juma lakini, walikiona kilichomtoa kanga manyoya.Walizabwa mabao 2:0 na Schalke 04.
Mabingwa Munich hawakuona mlango uwanjani mwao allianz arena walipokutana na viongozi wa Ligi Nüremberg hapo jumamosi.
Ingawa Munich,ilitamba nyumbani,Nüremberg, iliweza kuondoka suluhu 0:0 na kubakia kileleni kama viongozi wa Ligi.
Jana, Hamburg, ilioteremka na stadi wao mpya wa Holland, Joris Mathijsen,walitangulia kwa bao la Boubackar Sanogo,lakini Hertha Berlin,iliwaambia kutangulia si kufika.Walisawazisha na kugawana pointi.
Katika Ligi ya Uingereza-Premier League, Chelsea-mabingwa waliilazaba jana Blackburn 2:0 .
Kwanza, alikua Frank Lampard alietia bao la penalty,kabla ya muivory Coast,Didier Drogba kupachika bao la pili.Ushindi wa Chelsea, umekuja siku 3 tangu walipozabwa mabao 3-2 na Middlesbrough.
Nae kocha Jose Mourinho wa Chelsea, amemtuhumu kocha wa Ufaransa Raymond Domenech kwa kumfanyia Claude Makelele kama mtumwa.
Makelele aliekua akiichezea Real Madrid ya Spain, anakabiliwa na kufungiwa kucheza mechi 4 nchini Ufaransa, ikiwa hatawasili kujiunga na timu ya taifa ya Ufaransa kwa changamoto zijazo za kuania tikiti za finali ya kombe la Ulaya dhjidi ya Georgia na Itali mwezi ujao.
Claude Makelele, aliliarifu shirikisho la dimba la Ufaransa, azma yake ya kustaafu kuichezea timu ya Taifa ya Ufaransa,makamo-bingwa wa dunia.
Lakini, kocha Domenech na shirikisho la dimba la Ufaransa, wamekataa kuitikia uamuzi huo wa Makelele ; na kocha wake wa Chelsea,Mourinho anadai wafaransa sasa wanamuingilia Makelele katika haki zake za binadamu kwa kumtishia kumfungia kucheza .
Mwishoni mwa wiki hii, kinyan’ganyiro cha vikombe 2 vya Afrika kilikuwa uwanjani huku maandalio kwa changamoto za mwishoni mwa wiki ijayo kwa kombe la Afrika la mataifa yakisonga mbele:
ASEC Abidjan ya Corte d’Iviore,ilitamba kwa mara ya pili jana mbele ya enyimba ya Nigeria .Baada ya kuizaba mabao 3 ugenini katika duru ya kwanza, ASEC jana iliizima Enyimba nyumbani Abidjan kwa kutoka nayo sare 0:0.
Matokeo hayo yameifanya ASEC kuongoza kwa pointi 3 mbele ya Enyimba ikiwa kileleni mwa Kundi B na yaelekea kucheza nusu-finali mwezi ujao.Kwani, ASEC haikushindwa hata mara moja katika duru hii huku mechi 2 tu zikisalia.Enyimba imezimwa mara 2 sare tena nyumbani na matumaini yake sasa yamefifia.
Orlando Pirates ya Afrika Kusini,imefufua matumaini yake katika kombe hili baada ya ushindi wa bao 1:0 nyumbani mwa Hearts of oak huko Obuasi,Ghana hapo jana.Bao la orlando lilitiwa na mshambulizi wa Jamhuri ya kidemokrasi ya Kongo Blaise Mbele mnamo dakika ya 57 ya mchezo.
Pirates waliotoka sare nechi zao 3 zilizopita wana jumla sasa ya pointi 6 na hivyo moja zaidi kushinda Enyimba ya Nigeria.
Mabingwa al Ahly waliizaba Asante kotoko ya Ghana mjini cairo mabao 4:0.
Aka katika changamoto za kombe la shirikisho la dimba la Afrika ,etoile du Sahel ya Tunisia imetamba kwa mara ya pili mfululiuo ilipoitimua jana Renaicimento ya Guinea ya Ekweta mjini Malabo kwa mabao 2:0.Hapo jumamosi timu nyengine ya Tunisia-Esperence ilishinda kwa bao 1:0 nyumbani dhidi ya FC St Eloi Lupopo ya J.K.Kongo.
Timu kadhaa za Afrika zinajiwinda kwa changamoto za mwishoni mwa wiki ijayo za kuania tiketi za finali ya Kombe la Afrika la mataifa 2008 nchini Ghana.Tanzania, ni miongoni mwao na baada ya kumuajiri kocha mpya kutoka Brazil,Taifa Stars, wana miadi na Burkina Faso, mjini Dar-jumamosi hii ijayo kama vile mwanamichezo wetu Aboubakar
RIADHA:
Katika medani ya riadha,mabingwa wa Afrika walitamba jana huko Rieti,Itali:
Mkongomani Gary Kikaya alinyakua ushindi wa mbio za mita 400 wanaume wakati muafrika Kusini Mbulaeni Mulaudzi alinyakua ushindi wa mbio za mita 800 wanaume.Nafasi ya pili hapo alichukua mkenya Wilfred Bungei.
Ama katika mbio za mjita 1500,Bernard Lagat ,muamerika mzaliwa wa kenya, alitamba katika masafa hayo huku Tarek Boukensa wa Algeria akimfuata nafasi ya pili.
Katika zahama ya mbio za mita 300 wakenya na waethiopia walipapurana vikali na mwisho, mkenya Isaac Songok alikimbia muethiopia Tariku Bekele na kumuacha nafasi ya pili.Boniface Songok pia wa Kenya, alibidi kuridhika na nafasi ya tatu.
Ushindi katika mbio za mita 800 wanawake ulikwenda kwa msichana wa Kenya Janeth Jepkosgei.
Mbio za mita 3000 kuruka viunzi wanawake, Jeruto Kiptum wa Kenyxa alibidi kuridhika na nafasi ya pili huku ushindi ukienda kwa wioletta Janowska wa poland.Salome Chepchumba alimaliza 3.
Wakati wanariadha wa Kenya wakijinoa hapo kwa changamoto ya jumapili ijayo ya goldean League-mjini Berlin, polisi mjini nairobi, imemtia nguvuni raia wa Zambia alietaka kumpora fedha waziri wa michezo wa Kenya Maina Kamanda.
Kamanda alipokea simu kutoka Monaco kutoka mtu aliedai ni rais wa shirikisho la riadha duniani IAAF,Msenegal Lamine Diack.Mtu huyo alimuomba waziri huyo kutoa msaada wa dharura kwa mwanawe wa dala kiasi cha 5,100 akidai alitekwanyara na matokaa yake huko mombasa na kuibiwa kila alicho
kuanacho.
Waziri wa michezo wa Kenya alipompigia simu Lamine Diack,rais wa IAAF kujua iwapo angehitaji msaada zaidi kwa mwanawe,Diack alikanusha kujua chochote juu ya ombi hilo.Polisi nchini kenya imearifu itamfungulia mashtaka Banda kwa kujaribu kumfanyia ujambazi waziri wa michezo wa Kenya.
Mwishoe, mbio za magari za Grand Prix:Michael Schumacher wa Ujerumani,anaamini kwamba ataweza mwishoe kumpiku Fernando Alonso, na kunyakua kwa mara nyengine ubingwa wa mwaka huu wa formula One.Kuna mwanya wa pointi 12 kati yao huku mashindano 4 tu yakisalia.