1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KOMBE LA KLABU BINGWA LA AFRIKA

25 Julai 2005

KOMBE LA KLABU BINGWA AFRIKA:

Sare mjini Abidjan na Cairo ziliseleleza jana mtindo wa kuachana suluhu katika kundi B la kinyan’ganyiro cha mwaka huu cha kombe la klabu bingwa barani Afrika.Al Ahli ya Misri lakini, inahitaji ushindi mmoja tu kukata tiketi yake ya nusu-finali ya Kombe hili.

ASEC Abidjan ya Ivory Coast ilizimwa nyumbani kwa bao 1:1 na Etoile Sahel ya Tunesia wakati Esperence klabu nyengine ya Tunesia iliondoka sare bao 1:1 na Zamalek ya Misri.

Matokeo hayo 2 yaliomalizika sare yana maana kuwa ,mashindano ya kundi hili yamewasili sasa nusu-njia bila hata moja kati ya timu hizo 4 za kujipatia alao ushindi mmoja.

Zamalek inaongoza kundi hili kwa kuwa tu imetia mabao zaidi.Esperence ilisawazisha karibu na kipindi cha mapumziko pale nahodha wao Moyin Chaabani alipotia bao kwa kichwa.

Etoile sahel iliondoka na pointi kutoka Abidjan

Kwa BAO LA mkwaju wa penalty :

Bao la Sahel alilitia Bassem Ben Nasri mnamo dakika ya 86 ya mchezo.Asec Abidjan ilitangulia mnamo dakika ya 17 ya mchezo kutia bao .

Kinyume na kundi B la kuachana sare, kundi A,lilitoa washindi 2:Al Ahli ya Misri iliitandika Ajax cape Town na sasa wamebakisha ushindi mmoja tu kujitosa katika nusu-finali ya Kombe hilo la klabu bingwa.

Ahmed El Sayed ndie alietia bao la kwanza la Al Ahli mnamo dakika ya 8 ya mchezo.

Raja Casablanca ilitia bao mnamo dakika ya 80 ya mchezo kuizamisha jahazi ya klabu bingwa enyimba ambayo sasa inaburura mkia wa kundi hili.Pigo hilo limezika matumaini ya Enyimba kutwaa taji la klabu bingwa mara ya tatu mfululizo.

Ama katika zahama ya kuania Kombe la shirikisho la dimba la Afrika-CONFEDERATION CUP, mabingwa wa kombe hilo- Dolphin FC ya Nigeria, ilitia bao dakika za mwisho kuipiga kumbo Arab Contractors ya Misri.Dolphin ilishinda kwa mabao 2:1.Dolphin sasa inasimama kileleni mwa Kombe hili pamoja na Ismailia klabu nyengine ya Misri.King Feisal ya Ghana iliilaza Fello Star Labe kutoka Guinea kwa bao 1:0 mjini Conackry.

Finali ya Kombe la Castle Cup, la shirikisho la COSAFA itachezwa katika mji wa Mamabatho, Afrika Kusini.Nchi 4 zinashiriki katika mashindano haya ya siku 2 kuamua bingwa.Mabingwa watetezi Angola,wanaotumia changamoto hii kujinoa kwa mpambano wao wa mwisho wa kukata tiketi ya Kombe lijalo la dunia, wana miadi na Zimbabwe katika nusu-finali ya kwanza hapo August 13.Wenyeji Afrika Kusni wataumana na Zambia.Washindi watakutana siku ya pili kwa finali.Timu zote 4 ni washindi wa zamani wa kombe hili la COSAFA ambalo limekuwa likianiwa tangu 1997.

Wakati timu hizo 4 zajiandaa kwa Castle Cup, Simba ya Tanzania yajinoa kwa Kombe la Tusker huko Nairobi,Kenya.Sim,ba imeshawasili Nairobi .

Kenya itabidi kucheza mpambano wake ujao wa kuania tiketi ya Kombe la dunia 2006 bila ya watazamaji uwanjani-hii ni kwa muujibu wa uamuzi wa FIFA.

Timu ya mpira ya volleyball ya Kenya ilikata jana tiketi ya Kombe la dunia nchini Japan baada ya kuipiga kumbo Algeria kwa seti 3-2 ukumbini Kasarani,Nairobi .

Muamerika Lance Amstrong jana alitawazwa kwa mara ya 7 bingwa wa mbio za baiskeli za tour de France.Akivaa jazi ya manjano baada ya hatua ya 21 na ya mwisho,Amstrong alikimbia mbio zake za mwisho na sasa ana staafu.Ushindi wa hatua ya mwisho ya km 144 ulinyakuliwa na Alexandre Vinokourov wa Kazakhstan.Mjerumani Jan Ullrich amemaliza 3.

Katika medani ya riadha:

Bingwa wa olimpik wa masafa ya mita 1500 na 5000,mmorocco Hicham El Gerrouj ameamua kutoshiriki katika mashindano ya mwezi ujao ya ubingwa wa riadha ulimwenguni mjini Helsinki,Finland.El Gerrouj hakukimbia katika mashindano yoyote tangu ushindi wake katika michezo ya Olimpik,mwaka jana.

Na katika mashindano ya kuogolea ya ubingwa wa dunia mjini Montreal,Kanada, muafrika Kusini Roland Schoeman amevunja rekodi ya dunia wakati wa nusu-finali ya masafa ya mita 50 mtindo wa kipepeo.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW