Kombe la UEFA larudi uwanjani jioni hii
15 Februari 2007Leverkusen iliitimua nje Blackburn Rovers ya Uingereza na Werder Bremen Ajax Amsterdam ya Uingereza.
Al Ahli ya Misri, mabingwa wa Kombe la klabu bingwa barani Afrika, wataania Super-Cup jumapili hii wakipamabana na Etoile du Sahel ya Tunisia mjini Addis Ababa.
Jioni hii ni zamu ya mabingwa wa zamani wa kombe la UEFA Steua Bucharest ya Rumania kuumana na Sevilla ya Spian wakati Spartak Moscow ina miadi na Celta Vigo pia ya Spian.New castle United ya uingereza imefunga safari nyumbani mwa Zulte Waregem wakati Braga inaumana na Parma.Changamoto za jioni hii zakamilishwa kwa mpambano kati ya Racing Lens na Panathinaikos.
Jana klabu 2 za Ujerumani zilitimua vumbi kweli:bayer Leverkusen iliitimua Blackburn Rovers ya Uingereza kwa mabao 3:2.
Werder Bremen waliorudi nyuma katika kinyan’ganyiro cha Bundesliga-ilizaba Ajax Amsterdam mabao 3-0 na ina kila matumaini ya kutamba katika duru ijayo ya timu 16 za mwisho.
Arsenal london ilihitaji kurefushwa mchezo kabla kuitimua Bolton Wanderers jana na kuwasili duru ya 5 ya Kombe la FA la Uingereza.
Jogoo la Brazil,Ronaldo anatazamiwa jumapili hii kuvaa jazi kwa mara ya kwanza ya AC milan akiingia uwanjani kuania pointi 3 katika serie A-ligi ya itali.AC Milan klabu yake mpya inachuana na Siena.
Jumapili hii asie na mwana aeleke jiwe na asie na mguu atie gongo-mkutano mjini Addis Ababa:Baada ya kutawazwa mabingwa wa kombe la klabu bingwa barani Afrika-champions League, Al Ahly ya Misri inalitaka kombe la Super Cup la Afrika.Wabishi wake ni Etoile du Sahel ya Tunisia –mabingwa wa kombe la CAF-shirikisho la dimba la Afrika.
Oktoba mwaka jana ushindi wa kombe la klabu bingwa kwa Al Ahly ulisawazisha rekodi ya mahasimu wao wa nyumbani Zamalek wa kushinda mara 5 na wakiibuka washindi jumapili hii katika super cup,watasawazisha rekodi nyengine ya Zamalek.