KOMBE LA UEFA LEO UWANJANI
3 Novemba 2005· Baada ya changamoto za jana za champions League-kombe la klabu bingwa barani Ulaya,leo ni zamu ya Kombe la UEFA-kombe la shirikisho la dimba la Ulaya.Uwanjani ni klabu 2 za Ujerumani-Hamburg inamenyana na Viking Stavanger ya Norway wakati Stuttgart ina miadi na Shakhtar Donetsk ya Ukraine.
Mabingwa wa Ujerumani Bayern Munich jana walikiona cha mtema kuni walipozabwa mabao 2:1 na Juventus ya Itali.
· Ujerumani itakumbana na Ufaransa Novemba 9 kwa mpambano wa kirafiki,na kwa changamoto hiyo,Ufaransa imemuita kwa mara ya kwanza tangu kupita miaka 3, Nicolas Anelka na Roger Lemerre -kocha wa mabingwa wa Afrika- Tunisia amewateua wachezaji 3 wapya kwa changamoto na simba wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo huko Colombes,nje ya Paris, Ufaransa novemba 11.
· Stuttgart haimudu kulazwa tena leo na Donetsk ya Ukrain katika Kombe la UEFA.P igo jengine leo laweza likamkata kichwa kocha wao –mtaliana Giovanni Trappatoni.
· Hamburg inacheza nyumbani ikiwakaribisha wanorway-Stavanger na wana kila matumaini ya kutekeleza jukumu kwamba, “mcheza kwao, hutunzwa.”
· Mapambano mengine jioni hii katika Kombe hili ni kati ya Slavia Prague ya Jamhuri ya Czech na CSKA Sofia ya Bulgaria;Racing Lens ya Ufaransa na Halmstad ya Sweden.Sevilla ya Spain na Besiktas ya Uturuki.
· Jana katika champions League, mabingwa wa Ujerumani-Bayern Munich walikumtwa mabao 2-1 na Juventus ya Itali.Mabao 2 ya David Trezequet-la kwanza mnamo dakika ya 61 ya mchezo na la pili baadae, yalitosha kuirejesha Munich nyumbani mikono mitupu.Hatahivyo, bado Bayern Munich ina matumaini ya kutamba katika champions League,kwani huo haukuwa msumari wa mwisho katika jeneza lao.Juventus iko sasa kileleni mwa kundi hili A.Munich ina miadi sasa na Rapid Vienna Novemba 22 kabla haikufunga safari desemba 7 ya kwenda Bruges,Ubelgiji.
· Kiasi cha tiketi 150,000 za viti bora kabisa vya Kombe lijalo la dunia pamoja na tiketi za finali Julai 9 bado hazikuuzwa sokoni.Bei za tikiti hizo lakini zinaanzia dala 2,281.Kampuni la Uswisi ISE-Hospitality ndilo lenye haki ya kuuza jumla ya tiketi 336,000 za kombe lijalo la dunia.
· Kwa kujiandaa kwa Kombe hilo basi, wenyeji-Ujerumani wana miadi Novemba 912 ya kucheza na Ufaransa, mabingwa wa dunia, 1998.Kwa kujiandaa basi kwa changamoto hiyo, Ufaransa imemteua kujiunga na kikosi cha Taifa, staid wao wa zamani Nicolas Anelka anaecheza katika Ligi ya Uingereza na hii haikutazamiwa.Ufaransa itakumbana kwanza na
· Costa Rica kisiwani Martnique na Ujerumani mjini Paris katika uwanja wa Stade de France, Nov.12.
· Kocha wa mabingwa wa Afrika-Tunisia-mfaransa Roger Lemerre amewateua wachezaji 3 wapya katika kikosi cha Taifa kwa mapambano kadhaa ya kirafiki mwezi huu.Nao ni Sofiene Melliti na Hathem Mrabet.Watateremshwa uwanjani kupambana na samba wa jamhuri ya kidemokrasi ya Kongo nje ya Paris huko Colombe Nov.11.Mwengine ni staid wa etoile Sahel ya Tunisia-Chaker Zouaghi atakaeteremka uwanjani wakati wa mpambano na Misri mjini cairo, siku 5 baadae.
· Bingwa wa Olimpik wa Zimbabwe katika hodhi la kuogolea Kirsty Coventry atashiriki katika mashindano ya kuogolea ya Kombe la dunia ya FINA mjini Sydney,Australia mwezi huu.Coventry atajiunga huko na Muafrika Kusini Ryk neethling.mashindano hayo ya kuogolea yataanza Nov 19-20.