Kombe la UEFA na klabu bingwa ya dunia
16 Desemba 2008Kombe la dunia la klabu bingwa linalojumuisha timu 7 kutoka mabara yote linaendelea kesho huko huko Tokyo,Japan.Kabla mabingwa wa Ulaya Manchester United kuteremka uwanjani kupambana na wenyeji Gamba Osaka,Sir Alex Ferguson, kocha wa Manu amewataka wachezaji wake kuweka ukumbusho kwa kuifanya Manchester United klabu ya kwanza ya Uingereza kutawazwa mabingwa wa kombe hilo la dunia. Afrika inawakilishwa na mabingwa wake Al Ahly ya Misri ambayo kama Manchester itakuwa kesho uwanjani.
Barani Ulaya kinyanganyiro cha kuania nafasi ya timu 32 bora katika kombe la ulaya la UEFA kinaendelea leo na kesho huku waakilishi wa Ujerumani Hertha Berlin wakihitaji ushindi na Stuttgart haitatosha kutoka sare tu.
Nafasi 9 bado zikianiwa ili kujiunga na kundi la timu 32 za duru ijayo za kombe la Ulaya la UEFA lłeo hii na kesho, timu za Ujerumani katika Kombe hili zimekumbwa na shida:Hertha Berlin inahitaji ushindi ,kubakia mashindanoni wakati wenzao Stuttgart hata wakitoka sare haitatosha.Schalke inabidi kutumai wapinzani wao katika kundi lao hawashindi.
Hamburg na mabingwa wenzao wa zamani wa Ulaya Aston Villa wana miadi ya kuamua nani anatoka na nani anabakia.Mabingwa wa 2007 wa kombe hili Inter Milan ya Itali wana miadi na Wolfsburg katika changamoto ya timu zulizokwishakata tiketi zao za duru ijayo lakini zaania heshima tu ya nani anaibuka kileleni mwa makundi yao. Sare ingetosha kwa Wolfsburg ya Ujerumani ili kuibuka kileleni mwa kundi lao.
Mabingwa mara 2 wa kombe hili la Ulaya la UEFA Tottenham Hotsopur ya Uingereza pia ni miongoni mwa timu zinazoania kuingia duru ijayo ya kutoana itakayofikia kilele chake hapo kesho alhamisi.
Totteham ina shida zake pia-kuumia kwa wachezaji wake kadhaa.Mabingwa hawa wa Kombe la UEFA 1972 na 1984 wanauguliwa na mchezaji wao wa kiungo Jermaine Jenas wakati beki wao wa kati Jonathan woodgate hawezi kucheza n a halkadhalika nahodha Ledley King.
Huko Tokyo,Japan, kinyanganyiro cha kuamua ipi inaibuka klabu bingwa ya dunia kimeanza na kesho itakua zamu ya mabingwa wa ulaya Manchester united kuingia uwanjani kupambana na wenyeji Gamba United.Sir Alex Ferguson, kocha wa Manu analitamani kombe hili kwa kila hali ili M anu iandike historia kuwa klabu ya kwanza ya Uingereza kutawazwa mabingwa wa dunia. Jaribio lao la kwsanza mwaka 2000 lilizimwa na Vasco de Gama ya Brazil. Mara hii lakini Manu imejiandaa barabara na hii imeongoza kwa magazeti ya Uingereza kumkosoa Sir Alex kutia maanani zaidi kombe hili la dunia kuliko taji la nyumbani la Premeir League ambako Liverpool inaongoza na Chelsea ikifuata.
1999 Manchester United ilitwaa kombe la mabara 2 Intercontinental Cup lililoaniwa kati ya timu za Amerika kusini na Ulaya kabla ya kombe hilo kugeuka kombe la dunia la klabu bingwa.
Kwahivyo, Sir Alex amewataka mastadi wake waliopo Tokyo kuweka ukumbusho kwa kurudi Manchestedr City mara hii na kombe hilo ili kuandika historia kuwa timu ya kwanza ya Uingereza kuvaa taji la dunia chini ya enzi yake.
Mwishoe, taarifa kutoka Bundesliga-zasema stadi wa zamani wa timu ya taifa ya Ujerumani na naibu kocha wa Borussia Monchengladbach, Christian Ziege ameacha wadhifa wake kama naibu wa kocha .Ziege amekuwa naibu wa kocha Hans Meyer alieteuliwa hapo oktoba pale Borussia ilipoanza kuyumba yumba na sasa hali haikubadilika kwani, inaburura mkia.