KOMBE LA ULAYA LA MATAIFA
28 Juni 2004KOMBE LA ULAYA LA MATAIFA:
JAMHURI YA CZECH YAKATA TIKETI YA NUSU-FINALI YA KOMBE HILI
-KWANINI TIMU KUBWA-MABINGWA UFARANSA,UJERUMANI,ITALI,UINGEREZA,SPAIN ZILIAGA KOMBE HILI NA MAPEMA ?
Kombe la Ulaya la mataifa linapumzika leo na kesho likirudi uwanjani jumatano kwa nusu-finali ya kwanza baina ya wenyeji ureno na Holland ilioshinda majuzi changamoto ya mikwaju ya penalty dhidi ya sweden.
Jana Jamhuri ya Czech iliizaba Denmark,mabingwa wa zamani wa Kombe la ulaya mabao 3:0 na kukata tena gtiketi yao ya finali ya kombe hili kwa mara ya tatu baada ya 1976 ilipoilaza Ujerumani mjini Belgrade na kutwaa Kombe na 1996 ilipopokonywa Kom be na Ujerumani uwanjani Wembley,Uingereza.
Stadi wa Jamhuri ya Czech Milan Baros ndie anaeongoza orodha ya watiaji magoli. chipukizi huyo anaeichezea FC liverpool ya uingereza alitia jana mabao 2 kufuatia bao la kwanza la Jan Koller anaeichezea Borussia Dortmund katika Bundesliga.
Kocha wa Denamark Morten Olsen baada ya changamoto ya jana amesema timu yake imelipa gharama kubwa kwa kufanya madhambi ya kipumbavu.Wadeni waliwadhibiti wacheki hadi dakika ya 49 ya mchezo pale Jan Koller alipolifumania lango lao kwa kichwa.Iliosalia ilikua kazi ya chipukizi Milan Baros kuwachezesha wadeni kindumbwendumbwe na kujiandikia binafsi historia katika Kombe hili la Ulaya akiahidi katika mapambano 2 yaliosalia mabao zaidi.Wacheki wameshinda mechi zao zote 4 hadi sasa na katika nusu-finali ya pili maadui zao watakua Wagiriki chini ya kocha mjerumani Otto Rehagel.
Kwahivyo, timu 4 za mwisho katika Kombe hili la timu 16:ni Ureno na holland na Jamhuri ya Czech na Ugiriki.Zipi 2 zitakata tiketi yao kwa finali yajumapili ijayo-Julai 4 ni vigumu kwa sasa kubashiri na ilikuaje timu kubwa kubwa maarufu kama mabingwa Ufaransa,makamo-bingwa wa dunia-Ujerumani ,mabingwa wa Ulaya 2000Itali,mabingwa wa 1964 wa Ulaya Spain kupigwa kumbo na mapema nje ya Kombe hili ?
Dr.Abdullah Liki,mjumbe wa Barauza la michezo nchini Tanzania n a mchambuzi wa dimba anasema kuwa na wachezaji nyota tu leo haitoshi.Timu inatakiwa ionane na kuwa wachezaji wanacheza kitimu na kwa ari.Hii inaziba lile pengo la zile timu kubwa zenye wachezaji nyota kama Ufaransa,Uingereza,Ujerumani na Itali.
Nchi ndogo kama Latvia ilioisumbua Ujerumani imeziba mwanya kwa njia hiyo na Ugiriki ilikua vivyo hivyo.
Taarifa kutoka Afrika Kusini leo zasema wakuu mbali m bali maarifu wa dimba pamoja na marifu kadhaa wamefikishwa leo mahkamani kujibu mashtaka ya hongo au rushua kuhusu kupanga matokeo katika Ligi za daraja ya kwanza na ya puili za nchi hiyo-mwenyeji wa Kombe la dunia 2004.Miongoni mwa marifu hao wako wale wa FIFA.Pia mjumbe wa Halmashauri ya marifu ya Afrika Kusini ilikuwa nae nguvuni.