1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KOMBE LA ULAYA LA MATAIFA

1 Juni 2004

MICHEZO 31-05-04 MACHO YA WALIMWENGU YAKODOLEWA CHANGAMOTO YA JUMATANO KATI YA BRAZIL

NA ARGENTINA

-KOMBE LA KLABU BINGWA BARANI AFRIKA:ENYIMBA YAILAZA PETRO ATLETICO MABAO 2-1

ITALI IKIJIANDAA KWA KOMBE LA ULAYA LA MATAIFA IMEWALAZA MABINGWA WA AFRIKA TUNISIA 4:0

NA MKENYA ELLY RONO ASHINDA MBIO ZA MARATHON NCHINI KANADA

Macho ya mashabiki wa dimba ulimwenguni yatakodolewa keshokutwa jumatano mjini Belo Horizonte,Brazil ambako mabingwa hao wa dunia wataikaribisha Argentina katika kinyan’ganyiro cha kuania tikiti ya Kombe lijalo la du nia hapa ujerumani mwaka 2006 kanda ya Amerika kusini.

Argentina inaongoza orodha ya timu za kanda hii ikiwa na jumla ya pointi 11 kutoka mapambano 5 wakati Brazil inasimama nafasi ya tatu ikiwa na pointi 9.Timu 4 za usoni ndizo zinazotia tikiti zao kibindoni kuja ujerumani kwa Kombe la dunia 2006.Timu ya 5 ina nafasi ya kukata tiketi yake kwa kombe hilo la dunia kupitia mpambano maalumu.

Brazil na Argentina zimetwaa Kombe la dunia kwa pamoja mara 7.Kocha wa Brazil Carlos Alberto Parreira ameiona timu yake ikinyanyuka hivi karibuni kufuatia kutoka sare na mabingwa wa ulaya Ufaransa 0:0,imeichapa hungary mabao 4:1 na ikaizaba timu ya mchanganyiko ya Catalonia,Spain kwa mabao 5-2. Hatahivyo, Ronaldo –mshambulizi wa Brazil anasema hawatazamii mteremko mbele ya maadui zao na kwahivyo wanajiwinda barabara kwa cxhangamoto hiyo.

Tayari hapo kesho timu nyengine za kanda hii ya Amerika Kusini zinaingia uwanjani kuania nazo tiketi zao za kuja Ujerumani kwea kombe la dunia:

Mjini La Paz, wenyeji Bolivbia wanacheza na Paraguay.

San Cristobal, Venezuela inaumana na Chile na mjini Montevideo,wenyeji Uruguay wanapambana na peru.Jumapili ijayo Brazil itarudi uwanjani kupambana na Chile mjini Santiago.Argentina itakua nyumbani Buenos Aires ikiikaribisha Paraguay.

KABUMBU LA OLIMPIK 2004:

Matumaini ya ujerumani ya kukata tiketi ya dimba la michezo ijayo ya Olimpik mjini Athens,Ugiriki yameingia msukosuko baada ya kulazwa jana timu yao chini ya umri wa miaka 21 mabao 2-1 na Sweden.

Wajerumani walioanza uzuri dimba hili kwa kuikomea Uswisi mabao 2.! SASA WATAHITAJI ALAO KUTOKA SARE KATIKA MPAMBANO WAO UJAO NA NA WA MWISHO NA Ureno jumatano hii kubakisha matumaini ya kucheza katika dimba la Olimpik.Timu 2 za usoni kutoka kila kundi zaingia nusu-finali.

Ureno wenyeji wa kombe lijalo la Ulaya la mataifa wa mechafua nafasi zao walipomudu suluhu tu 2:2 na Uswisi mjini Mainz, ujerumani.

Bila kujali Kombe lijalo la Ulaya la mataifa linaloanza chini ya wiki 2 kutoka sasa nchini Ureno litamalizika kwa ushindi wa nanani,kwa mabingwa wa Ulaya Ufaransa mashindano yajayo yatamaliza kizazi cha wachezaji waliokuja juu chini ya kocha wa zamani Aime Jacquet.Mnamo muda wa miaka 10 ,Uufaransa, ndio timu bora kabisa ya dimba kutoka Ufaransa.

kizazi hiki kimekua cha kwanza kunyakua kombe la na la Ulaya kwa Ufaransa kabla haikupata pigo kali kabisa katika kombe la dunia katika historia ya Ufaransa kwenye Kombe hilo.walilazwa na Senegal na baadae kutolewa duru ya kwanza.

Ufaransa ikiteghemea mastadi wake akina Zinedine Zedane na Thierry Henry, inapigiwa tena upatu kuwika katika kom,be hili la dunia nchini Ureno.

Wenyeji lakini Ureno chini ya kocha wa zamani wa Brazil felipe Scolari waweza pia kulizuwia kombe hilo kuondoka na hasa kbaada ya ushindi wao wa FC Porto katika kombe la Ulaya la klabu bingwa wiki iliiopita.

Itali ilijipioma nguvu jana kwa kuwalaza mabingwa wa afrika tunisia mabao 4:0 na hivyo kama Ujerumani ilioilaza Malta mabao 7:0 kati ya wiki iliopita,haifai kuwatoa maanani.

Katika Kombe la klabu bingwa barani Afrika, Enyimba ya Nigeria,mabingwa wa kombe hilo walitia jana bao la dakika ya mwisho na kuilaza Petro Atletico ya Angola mabao 2:1 na hivyo imenyakua tiketi yake ya kuingia duru ijayo.

Esperence ya tunisia iliitoa Contonsport Garoua ya Kamerun kwa bao 1:0.Supersport United ya afrika kusini ikicheza mara ya kwanza katika Kombe hili imetoka sare 0:0 na Al Hilal ya Sudan mjini Oumduraman.

Timu 8 zilizovuka salama sasa zitagawiwa makundi 2 hapo Juni 8 itakapopigwa kura jinsi zitakavyopambana.Nazo ni Africa Sports,Bakili Bullets ya malawi,Enyimba ya Nigeria,Esperence ya tunisia,etoile du sahel püia ya tunisia,Jeanne d’Arce ya Senegal,Super Sport United ya Afrika kusini na USMa ya Algeria.

Mkenya Elly Rono alishinda jana mbio za marathon za National capital huko Ottawa,kanada.Moustapha Bennacer wa Algeria alikuja wapili huku Aldredo Arevalo Reyes wa Guatalama akishika nafasi ya tatu.

Michael Schumaceher wa Ujerumani, aliwika tena mwishoni mwa wiki kwa ushiundi wake katika mbio za magari huko Nueburgerring,Ujerumani. Huo ulikua ushindi wake wa 76 kwa jumla.

na kwa taarifa hiyo ya ushindi mwengine wa Michael Schumacher,ndio sina budi bali kuishia hapo kwa sasa.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW