1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KOMBE LA ULAYA LA MATAIFA:UINGEREZA YACHEZA LEO NA CROATIA NA UFARANSA NA USWISI.JAN URENO ILIPIGA KUMBO SPAIN.

Ramadhan Ali21 Juni 2004

MICHEZO 21-06-04

Baada ya Ureno na Ugiriki jana kukata tiketi zao za robo-finali zikiifuata Jamhuri ya Czech, mabingwa wa dunia –Ufaransa wanarudi uwanjani jioni hii wakipambana na Uswisi wakati Uingereza wataumana na Croatia.

Mshambulizi hatari wa Croatia Dado Prso ana yakini kwamba, Croatia itanguruma mbele ya waingereza na ni wao watakaotoroka na tiketi ya robo-finali , lakini amewaonya wenzake watarajie kazi ngumu uwanjani kuzima vishindo vya waingereza.Prso ndie alietia bao la pili la Croatia dhidi ya mabingwa wa Ulaya Ufaransa kabla Trezeague hakusawazisha kwa Ufaransa.

Ufaransa inaongoza wakati huu kundi B ikiwa na pointi 4,Uingereza 3 na Croatia wako nafasi ya 3 wakiwa na pointi 2 huku Uswisi ikiwa na 1.Croatia kwahivyo lazima ishinde leo ikiwa inataka kusonga mbele wakati waingereza itatosha wakitoka sare tu.

Wakati huo huo,Ufaransa itajitutumua kuona udhia ilioupata majuzi kutoka kwa wacroatia ,hauwakuti tena leo mbele ya Uswisi.

Wafaransa watataka kuondoka na pointi 3 ili kuondoa shaka-shaka zozote kwamba jahazi lao linaenda mrama na huenda likazama.

Zinedine Zedane, atakua tena ufunguo wa mashambulio yao n a pamoja na Thierry Henry na David Trezegue, wafaransa wanajiwinda kutamba tena uwanjani.

Jana Ureno nzima ilikua shangwe na shamra-shamra kana kwamba waremno wameshalitwaa Kombe la Ulaya la Mataifa.Ureno jana ikicheza kufa-kupona, ilirekodi ushindi wao wa kwanza dhidi ya majirani zao Spain wa bao 1:0.Ureno haikuthubutu kuilaza Spain tangu kupita miaka 23.kwahivyo jana ilikua asie na mwana aeleke jiwe na asie kua na mguu alitia gongo-sherehe uwanjani,mitaani na hata vijijini,wakubwa kwa wadogo,virembwe na vijukuu vilishangiria ushindi huo.Kila mahala ilikua ‘VIVA PORTUGAL’-iishi Ureno.

"Kwaheri Spain" kilikua kichwa cha habari katika gazeti la Correio da Manha.Ilikua Nuno Gomes alieitwa uwanjani alieufumania mlango wa Spain na kuupiga msumari wa mwisho katika jeneza lao katika Kombe hili la Ulaya.Mpambano wa jana ulikua kwa Ureno wa kufa kupona sio tu kwa timu yao bali hata kwa kocha wao-mbrazil.Laiti Ureno ingetolewa duru ya kwanza,basi shoka lililokua tayari linameta meta tangu Ureno kuzabwa mabao 2-1 na Ugiriki katika mpambano wa ufunguzi,lingemfyeka Felipe Scolari.

Ikiwa imetolewa maanani kwamba ni miongoni mwa timu zinazoshiriki tu na hazina lake jambo,Ughiriki mara hii imetia fopra alao hadi jana.kwani, ikishiriki kwa mara ya kwanza katika kombe la Ulaya la mataifa tangu kupita miaka 24, Ugiriki chini ya kocha wake mjerumani Otto Rehagel, imetoroka na tiketi yake ya kucheza duru ijayo ya robo-finali licha ya kuza