1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kombe la Ulaya la UEFA

15 Aprili 2009

Hamburg na Bremen na Donetsk na Kiev za ukraine ?

Diego-jogoo la Bremen.Picha: picture-alliance / dpa

Firimbi iatlia jioni hii kwa duru ya pili ya robo-finali ya Kombe la ulaya la UEFA-Kombe la shirikisho la dimba la Ulaya.Kuna uwezekano kwa timu 2 za Ujerumani na 2 za Ukraine kuingia nusu-finali ya kombe hili mradi tu Hamburg imetamba tena mbele ya Manchester City na Breemn inaipiga kumbo leo Udinese huko kwao Itali.Donetsk ya ukraine nayo inatetea mabao yake 2 nyumbani mwa Olympique Marseille .Dynamo Kiev iko nyumbani ikiikaribisha Paris st.Germain baada ya kutoka nayo suluhu duru iliopita ya bila kwa bila.

Tufungue zaidi pazia la changamoto za leo za Kombe la ulaya linalofuatia duru ya pili ya robo-finali ya jana usiku kati ya Manchester United na FC Porto na Arsenal na Vilarreal ya Spain:

Klabu 2 za Ujerumani-Hamburg na Bremen majirani wa kaskazini ndio timu 2 pekee zinazopepea bendera ya Bundesliga katika vikombe vya ulaya baada ya wenzao mabingwa Bayern munich kutimuliwa nje na FC Barcelona ya Spian. Munich ilifuta kashfa ya Barcelona ya mabao 4-0 kwa kumudu sare nyumbani ya bao 1:1.Manchester city na Udinese zinapaswa kufuta ushindi wa mabao 3-1 wa timu hizo mbili za ujerumani katika kinyanganyiro cha leo cha kuania nafasi ya nusu-finali. Hamburg ililaza Manchester city na Brtemen ikatamba mbele ya udinese.Manchester city na Udinese ni klabu 2 za mwisho za Uingereza na Itali katika Kombe la UEFA na wengi wanabashiri nusu-finali kwa timu 2 za Ujerumani na 2 nyengine za Ukraine. Moja kati ya hizo itacheza finali hapo mei 20,mjini Isttanbul,uturuki.Udinese ya itali lakini haikukata tamaa ya kuweza leo kuwatiia munda Bremen.kwahivyo, wabremen wachunge ili wembe uliokaribia kuwanyoa Chelsea walipocheza na Liverpool usije ukawanyoa wao.

Nahodha wa zamani wa Ufaransa na rais wa sasa wa UEFA-shirikisho la dimba la Ulaya,michel Platini,alidai jana kwamba timu 2 za ukraine Donetsk na Dynamo Kiev ni kali zaidi kuliko timu 2 za nyumbani Ufaransa-Paris st.Germain na Olympique Marseille, ikiwa hii ni kweli, tutajionea jioni hii baada ya firimbi ya mwisho kulia.

Shakhtar Donetsk inaitembelea Olympique Marseille ikiwa na mabao 2 mfukoni kutoka duru ya kwanza iliochezwa nyumbani Kiev wakati wenzao Dynamo wanaikaribisha leo Paris St.Germain ,baada ya kumudu nayo sare ya 0:0 wiki iliopita mjini Paris.

Platiini alikuwa Ukraine akiongoza ujumbe wa UEFA uliwasili huko kukagua maandalio ya Kombe lijalo la ulaya 2012 linaloandaliwa kwa ubia kati ya Ukrain na jirani yake Poland.

Katika duru iliopita, Tomas Huebschmann aliipatia Donetsk bao la kwanza dakika 6 tu baada ya kuanza dimba na kinyume kabisa na mkondo wa mchezo.Dontesk ikaongeza bao la pili katika kipindi cha pili pale mbrazil Jadson alipouona wavu wa Marseille.

Kocha wa Marseille katika mpambano ule wa kwanza Eric Gerets alidai kuwa Marseille ilicheza bora zaidi kipindi cha pili kuliko waukraine,lakini walitiwa bao na mapema.

Olympique Marseill ni mabingwa wa Kombe la ulaya la klabu bingwa-champions league mwaka 1993 walipotamba na mghana Abedi Pele na mara hii wanajaribu kuwasili finali ya kombe hili la UEFA kwa mara ya 3 tangu 1999.Wenzao Shakhtar Donetsk ya Ukraine wanajaribu kuingia nusu-finali ya kombe hili la ulaya kwa mara ya kwanza.

Mwandishi:Ramadhan Ali/ DPA/RTRE

Mhariri:M.AbdulRahman

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW