1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Komorowski ashinda uchaguzi wa rais Poland

5 Julai 2010

Bronislaw Komorowski, ameshinda duru ya pili ya uchaguzi wa rais uliofanywa siku ya Jumapili nchini Poland.

Parliament Speaker, acting president Bronislaw Komorowski with wife Anna enter a voting station in Mackowa Ruda, northeast Polan, Sunday, July 4, 2010. Poles are choosing their new president in the runoff presidential elections, between Komorowski and Jaroslaw Kaczynski, twin brother of the late President Lech Kaczynski who was killed in a plane crash.(AP Photo/Alik Keplicz)
Bronislaw Komorowski na mkewe Anna.Picha: AP

Kwa mujibu wa televisheni ya taifa TVP, Komorowski amejikingia asilimia 53 ya kura zilizopigwa wakati mpinzani wake, Jaroslaw Kaczynski amepata asilimia 47.

Kaczynski ni kiongozi wa chama kikuu cha upinzani kinachofuata sera za mrengo wa kulia, "Law and Justice" na ni ndugu pacha wa rais Lech Kaczynski alieuawa katika ajali ya ndege mwezi wa Aprili.Uchaguzi wa rais umeitishwa kufuatia kifo hicho.

Matokeo ya uchaguzi huo humaanisha kuwa Komorowski wa chama cha kiliberali cha "Civic Platform" na mshirika wake wa karibu, Waziri Mkuu Donald Tusk wataweza kuidhinisha marekebisho ya kifedha kabla ya uchaguzi wa bunge uliopangwa kufanywa mwakani.

Waziri Mkuu wa Poland,Donald Tusk.Picha: picture alliance/dpa

Kwa mujibu wa Katiba ya Poland, wajibu wa rais sio kuliwakilisha taifa tu bali ana mamlaka yake hasa katika sera za nje na usalama. Jaroslaw Kaczynski amekubali kuwa ameshindwa na amempongeza mpinzani wake Komorowski.

Mwandishi:P.Martin/RTRE/DPA

Mhariri: Mwadzaya,Thelma

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW