Kongamano la Kimataifa la Vyombo vya Habari
28 Juni 2015Miongoni mwa mada zilizojadiliwa ni usalama wa mitandao ya kijamii, sera za kigeni katika kuripoti mizozo ya kimataifa, matumizi ya mtandao wa mawasiliano wa intaneti barani Afrika na njia za kuulinda uhuru wa vyombo vya habari.
Unagana na Josephat Charo katika kipindi cha Maoni Mbele ya Meza ya Duara akiwa pamoja na Michael Andindilile, Mkuu wa Shule kuu ya Waandishi wa Habari na Mawasiliano ya Umma, Chuo kikuu cha Dar es Salaam, Tanzania. Simaloi Dajom Otieno, Naibu Mkurugenzi wa Vipindi, kampuni ya Royal Media Services, inayomiliki Redio Citizen, na Faustine Peter Nyanda, Mkuu na Muasisi wa asasi ya kimataifa inayojihusisha na masuala ya ulinzi na usalama Afrika na masuala ya uhamiaji, International Campaign for Africa, mjini Zurich Uswisi.
Kusikiliza maoni haya bonyeza alama ya spika hapo chini.
Mwandishi:Josephat Charo
Mhariri:Mohammed Abdulrahman