Kongamano la kimataifa mjini Bonn: Mahojiano na Anthony Diallo wa Tanzania
22 Juni 2010Kongamano la siku tatu la kimataifa juu ya vyombo vya habari lililotayarishwa na Deutsche Welle hapa mjini Bonn, Ujerumani, na lililoanza jana, limeendelea leo kwa kuwasikiliza wataalamu mbali mbali wanoshughulisha na masuala ya mabadiliko ya hali ya hewa duniani wakiwaarifu waandishi wa habari juu ya hatari zinazokabiliwa na wanadamu katika jambo hilo na namna ya kupata suluhisho la matatizo hayo. Hayo yatawasaidia waandishi wa habari kuwaarifu watu kwa lugha nyepesi juu ya changamoto hiyo.
Mmoja ya watu wanaoshiriki katika kongamano hilo ni Anthony Mwandu Diallo, mbunge wa Ilemela huko Tanzania, na pia mmiliki wa Radio Free Afrika na pia Televisheni ya Star huko Mwanza. Nini alichofaidika Bwana Diallo hadi sasa na kongamano hili, alimuelezea hivi mwenzangu Othman Miraji...