Kongamano la lugha ya Kiswahili lakamilika Bayreuth
2 Juni 2015Matangazo
Kongamano la siku tatu la kimataifa juu ya taaluma za Kiswahili limemalizika mchana wa leo (02.06.2015) katika mji wa Bayreuth, kusini mwa Ujerumani. Wataalamu na washiriki kutoka zaidi ya mataifa na vyuo vikuu 20 ulimwenguni wameazimia haja ya kuunganisha nguvu kukipa Kiswahili uthubutu na nafasi yake kinachostahiki kwenye ulimwengu wa sasa kwani tayari kimejipambanua chenyewe kuwa lugha inayoliwakilisha na kulisemea bara zima la Afrika.
Mohammed Khelef ambaye amekuwa akihuhudhuria kongamano hilo, ametutumia taarifa ifuatayo kutoka Bayreuth.
Kusikiliza ripoti bonyeza alama ya spika za masikioni hapo chini.
Mwandishi:Mohammed Khelef
Mhariri:Josephat Charo