1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Euro bilioni 2 zachangishwa kusaidia Sudan mjini Paris

16 Aprili 2024

Zaidi ya euro bilioni mbili za msaada kwa ajili ya Sudan zimechangishwa katika kongamano la wafadhili lililoandaliwa jana mjini Paris, Ufaransa.

Paris, Ufaransa I Kongamano la wafadhili wa sudan
Washiriki wa kongamano la wafadhili wa Sudan wakiendele na mkutano mjini ParisPicha: Bertrand Guay/REUTERS

Hii ni baada ya Ujerumani, Ufaransa na Umoja wa Ulaya kuiomba jumuiya ya kimataifa kutoa msaada wa dharura kushughulikia hali ya kutisha ya kibinaadamu katika nchi hiyo inayokumbwa na vita vya wenyewe kwa wenyewe. 

Rais Emmanuel Macron amesema wakati akiufunga mkutano huo jana jioni kuwa hawajasahau kinachoendelea Sudan. 

Amesema kiwango cha dhamira yao kitawawezesha kuyatimiza mahitaji ya dharura ya chakula, afya, maji, usafi, elimu na ulinzi wa watu walioko hatarini zaidi. 

Soma pia:Mataifa ya Ulaya yafanya kongamano kuichangia fedha Sudan

Akizungumza mjini New York, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema ulimwengu unawasahau watu wa Sudan na kutoa wito wa juhudi za pamoja za kufikiwa mpango wa kusitisha mapigano na kumaliza umwagaji damu.

Amesema njia pekee ya kumaliza mzozo huo ni suluhisho la kisiasa. 

Vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini Sudan vimeingia mwaka mmoja tangu vilipoanza Arili 15 mwaka jana.
 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW