Kongamano la wake wa marais Afrika lafikia tamati
11 Oktoba 2023Wataalam kutoka nchi tofauti na mashirika mbali mbali ya kimataifa waliwaelimisha washiriki katika kongamano la wanawake viongozi juu umuhimu wa kudhibiti kasi ya ongezeko la watu katika nchi nyingi za Afrika.
Nchi za Rwanda, Malawi na Zanzibar zimetajwa kuwa zimefanikisha uzazi wa mpango, na kushuhudia mabadiliko makubwa.
Akihitimisha shughuli za kongamano hilo, Bi Angeline Ndayishimiye mke
wa Rais ambaye kongamano hilo liliandaliwa na kituo anacho kiongoza ,
aliagiza katika kongamano litakalo fuata, waziri mkuu Gervais Ndirako
buja kuhakikisha wanashiriki wanawake na wanamume ili waweze
kubaddilisha maoni juu ya changamoto zinazo sababishwa na ongezeko la
idadi ya watu.
Soma pia:Uganda: Ruksa wasichana wadogo kutumia uzazi wa mpango
Kwa muda wa siku 3 za kongamano hilo la wanawake viongozi, miadhara
ilotolewa ilisisitisha juu ya umuhimu wa kuthibiti kasi ya ongenzeko la watu katika nchi nyingi za bara Afrika.
Baadhi ya nchi zapiga hatua ajenda uzazi wa mpango
Athanase Nzokirihisha mtaalam kutoka shirika la Umoja wa mataifa linalo huisika na ongenzeko la idadi ya watu, alisema nchi za Rwanda, Malawi na Ethiopia zimepiga hatua katika uzazi wa mpango.
Mfano ni nchi ya Malawi inaonesha utashi wa kisiasa katika kuchukua hatua kwenye suala zima la kushughulikia ongezeko la idadi ya watu.
Wakaazi wa nchi hiyo wanao tumia uzazi wa mpango wamefikia asilimia 68.6.
Mtaalam huyo aliongeza kuwa Palipo na watoto wengi, asilimia 30 ya miradi utekelezaji wake unasua sua, huku vijana wakikabiliwa na ukosefu wa ajira.
Bi Mariam Mwinyi mke wa rais wa Zanzibar alionesha filamu fupi ya kituo maisha Fondation anacho kiongoza.
Soma pia:Wake wa viongozi Afrika himizeni ajenda ya uzazi wa mpango
Kupitia kituo hicho wanawake wakulima wanaelemishwa juu ya uzazi wa mpango na kupewa mikopo ya kujiendeleza.
Kwa upande wake Daktari Ananie Ndacayisaba ambaye ni mkuu wa mpango wa
chanjo nchini, amesema Burundi raia wanatakiwa kuelemishwa vya kutosha juu ya umuhimu wa uzazi wa mpango.
Aliongeza kwambawakaazi wengi wanaimani kuwa kuwa na idadi kubwa ya watoto ni utajiri.
Shuhuli za Kongamano hilo ziliudhuriwa na wake wa marasi kutoka Rwanda, Zanzibar, pamoja na Maafisa kutoka mashirika ya Umoja wa mataifa.