1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
BiasharaUlaya

Kongamano la uwekezaji lafunguliwa mjini Berlin

20 Novemba 2023

Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz amewaalika viongozi wa mataifa ya Kiafrika na yaliyostawi kiviwanda ya kundi la G20 katika kongamano la wawekezaji mjini Berlin.

Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa akiongea na waandishi wa habari juu ya kongamano la uwekezaji Berlin.
Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa akiongea na waandishi wa habari juu ya kongamano la uwekezaji Berlin.Picha: Tobias Schwarz/REUTERS

Mkutano huo ulioanza leo ni sehemu ya dhamira ya serikali kuziunga mkono nchi za Kiafrika katika kupata mafanikio ya kiuchumi.

Waziri wa Uchumi wa Ujerumani Robert Habeck anahudhuria mkutano huo wa kilele, pamoja na Rais wa Halmashauri Kuu ya Umoja wa Ulaya Ursula von der Leyen, Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron, viongozi kumi wa mataifa ya Afrika na serikali, na zaidi ya mawaziri 30 kutoka barani humo.

Soma pia:Mkutano wa uwekezaji Afrika wafanyika Berlin

Heiko Schwiderowski, mkuu wa Chama cha wenye Viwanda na Biashara cha Ujerumani anayehusika namasuala ya kanda ya Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara, DIHK amesema kongamano hilo la uwekezaji lenye wajumbe 800 linaelezewa kuwa kongamano kubwa kabisa la kibiashara kuwahi kufanyika kwenye ardhi ya Ujerumani.

Schwiderowski anasema viongozi wa kibiashara na kisiasa nchini Ujerumani wanatuma ishara muhimu, akiongeza kuwa kupanua mahusiano ya kiuchumi ni jitihada yenye manufaa.