SiasaJamhuri ya Kongo
Kongo-Brazzaville yapiga kura katika uchaguzi wa rais
15 Machi 2026
Matangazo
Takribani wapiga kura milioni tatu wamejiandikisha kushiriki katika uchaguzi huo.
Hata hivyo, hali ya uchaguzi inaonekana tulivu hasa miongoni mwa vijana wengi ambao wanaamini kuwa rais huyo wa muda mrefu ataendelea kushinda. Vyama kadhaa vya upinzani pia vimetangaza kususia uchaguzi huo vikidai kuwa hauko huru na wa haki.
Kwa mujibu wa wachambuzi, wagombea sita wanaoshindana na Denis Sassou Nguesso hawana uwezo mkubwa wa kumzuia kuendelea kubaki madarakani. Rais huyo amekuwa madarakani kwa jumla ya miaka 42.
Uchaguzi huu unafanyika wakati nchi hiyo yenye utajiri wa mafuta inakabiliwa na madeni makubwa ya kimataifa na ukosefu mkubwa wa ajira kwa vijana. Zaidi ya nusu ya wananchi wa Jamhuri ya Kongo wanaishi katika umaskini.