Kongo kuendelea na kesi dhidi ya jaribio la mapinduzi
26 Juni 2024Mahakama hiyo imekataa jana Jumanne ombi la kutupilia mbali kesi hiyo, lililotolewa na mawakili wa upande wa watuhumiwa.
Mawakili hao waliitaka mahakama hiyo ya mjini Kinshasa kutangaza kwamba haina uwezo wa kuwashtaki watuhumiwa hao, ambao wote ni raia, kuhusiana na jaribio hilo lililoshindwa la mapinduzi, lililofanyika Mei 19 katika mji mkuu Kinshasa.
Waliohusika katika jaribio la mapinduzi Kongo kushitakiwa
Jaribio hilo linadaiwa kuongozwa na Christian Malanga, Mkongomani ambaye alikuwa na uraia wa Marekani japo aliuwawa na vikosi vya usalama vya Kongo.
Kadhalika mahakama hiyo ya Kijeshi imekataa ombi la kuwaachilia kwa muda watuhumiwa, akiwemo Jean-Jacques Wondo, mtaalamu wa masuala ya kiusalama wa Kongo mwenye uraia wa Ubelgiji, ambaye mwanasheria wake amesema anakabiliwa na matatizo ya kiafya.