1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kongo kupokea wahamiaji kutoka Marekani

5 Aprili 2026

Kongo itapokea baadhi ya wahamiaji kutoka Marekani kama sehemu ya makubaliano mapya chini ya mpango wa nchi ya tatu wa utawala wa Rais wa nchi hiyo Donald Trump.

USA Baltimore 2025 | muhamiaji
Watu wajitokeza kuomba na mhamiaji wa Salvador ambaye ni mkazi wa Marekani Akilmar Abrego Garcia ambaye serikali ya Marekani ilimhamisha kutoka nchini humo mnamo Agosti 25, 2025Picha: Roberto Schmidt/AFP

Katika taarifa, wizara ya habari ya Kongo imesema wahamiaji hao wataanza kuwasili nchini humo mwezi huu bila ya kutoa maelezo zaidi kuhusu tarehe ama idadi inayotarajiwa.

Taarifa hiyo imeendelea kusema kuwa mpangilio huo ni wa muda tu unaoonyesha kujitolea kwa Kongo kwa ubinadamu na mshikamano wa kimataifa.

Hata hivyo imesema serikali ya Marekani itasimamia gharama zote.

Serikali ya Kongo imesema hakuna uhamisho wa moja kwa moja unaopangwa, na kuongeza kuwa kila mhamiaji atakayeletwa nchini itachunguzwa kulingana na sheria za nchi hiyo na matakwa ya usalama wa taifa.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW