1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaJamhuri ya Kongo

Kongo: Mapigano yapamba moto kati ya jeshi na waasi wa M23

8 Novemba 2023

Mamia ya watu wamekimbia tena makaazi yao leo baada yakushuhudiwa kwa mapigano makali kati ya jeshi la Congo na waasi wa M23 waliozilenga kwa makombora ngome za jeshi wilayani Masisi.

Askari jeshi wakiwa katika doria Goma, Jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo
Askari jeshi wakiwa katika doria Goma, Jamhuri ya kidemokrasia ya KongoPicha: Alain Uaykani/Xinhua/picture alliance

Vyanzo vya kiraia pia katika eneo hilo, vimeeleza kuwa asubuhi ya leo kikosi cha jeshi la Burundi kiliteketeza moto baadhi ya vifaa vyake kwenye kambi yao ya mjini Kitshanga kabla kikosi hicho kuelekea katika sehemu isio fahamika.

Tangu alfajiri mapema kwenye ngome ya jeshi tiifu kwa serikali katikati mwa mji wa Kilolirwe ulio karibu kilometa 30 kutoka sake wilayani masisi.

Katika tangazo lao kwenye mtandao wa X , kundi hilo lilitangaza kuudhibiti  mji huo unaounganisha eneo hilo na Goma baada yakuteka pia milima ya Gicwe iliyokuwa ngome muhimu ya jeshi la Congo nakuendelea hadi mji mdogo wa Kausa.

Hadi jioni leo, mamia wa raia wanaokimbia wamiminika katika mji wa sake, kimometa 25 kutoka Goma.

Soma pia:Blinken azungumza na Kagame na Tshisekedi kuhusu M23

Wakati hayo yakiendelea, kikosi cha jeshi kutoka nchini Burundi kilichopelekwa kwenye eneo hilo ili kuleta utulivu, kimeteketeza kwa moto baadhi ya vifaa vyake ikiwemo zana za kivita katika kambi yao mjini Kitshanga.

Kulingana na vyanzo vya kiraia kumeongeza wasiwasi baada ya kikosi hicho kuondoka na kuelekea sehemu isiyofahamika.

Pande za mzozo zatupiana lawama

Waasi wa M23 kwa siku kadhaa, wamekuwa wakiwashutumu wanajeshi wa Burundi kwa kushirikiana na askari wa Kongo katika mapigano hayo yanayoendelea kusambaa.

Vita vya M23 vinaathiri pia wakazi wa Bukavu

02:40

This browser does not support the video element.

Tuhuma hizo zilikanushwa na serikali ya Burundi miezi michache iliyopita.

Hali hiyo ya wasiwsi pia ,ilishuhudiwa katika miji ya Buhumba na kibati wilayani Nyiragongo ambako ndege za kivita zilitumiwa na jeshi la Kongo kwa kuzibomoa kwa mizinga ngome za waasi wa M23.

Soma pia:Mapigano yaendelea mji wa Kitshanga Kongo

Mapigano yamesababaisha uharibifu mwingine wa waya zinazo sambaza umeme katika mji wa Goma siku moja baada waya hizo kufanyiwa marekebisho.

Sehemu kubwa ya mji wa Goma unaokaliwa na zaidi ya watu milioni moja imegubikwa na giza ambalo madhara yake yatakuwa mabaya zaidi.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW