1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kongo: Mishahara ya wabunge yapunguzwa ili kuleta usawa

Jean Noël Ba-Mweze
17 Juni 2024

Mishahara ya wabunge nchini Jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo imepunguzwa ili kuweka usawa wa baina ya malipo miongoni mwa wafanyakazi katika sekta ya umma, katika taifa hilo linalokabiliwa na mgogoro wa kiuchumi.

Kinshasa, DR Kongo | Siasa | pika wa Bunge Vital Kamerhe
Spika wa Bunge Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo Vital KamerhePicha: Arsene Mpiana/AFP

Kwa miaka mingi ndipo wabunge walikuwa wakipokea mshahara uliozidi ule wa watumishi wengine. Kwa hivyo ndoto ya kila mkongo ilibaki tu ni kuwa mubunge kabla ya kufa. 

Hatua hii ni kufuatia vuguvugu lililoendeshwa na wanasiasa kutoka vyama vya upinzania nchini humo ambao walitaka mishahara ya wabunge kupunguzwa ili kupunguza uzito wa matumizi ya fedha za umma.

Hata hivyo Wabunge waliendelea kupokea fedha ambazo kiasi hakikujulikana kamili hadi wakati mwanasiasa kutoka chama cha upinzani Martin Fayulu aliweka hadharani kiwango cha mshahara wa Mbunge ni dola ya Marekani elfu ishirini na moja (21.000).

Katika mkutano wa wabunge Jumamosi iliyopita, Spika wa Bunge Vital Kamerhe aliwaelezea kuwa mubunge sasa watapokea milioni 14 ya franka za Kongo, yaani dola elfu tano za Marekani kwa mwezi.

Soma pia:Bunge la Kongo laidhinisha serikali ya Waziri Mkuu Suminwa

Kamerhe pia aliwashukuru Wabunge kutokuwa na upinzani katika hatua hiyo ya serikali ambayo ina nia ya kushughulikia changamoto ambazo wananchi wanakabiiana nazo ikiwemo kupanda kwa gharama za maisha.

"Tuliahidi kwamba tutapunguza tofauti za mishahara. Halafu nawashukuru ninyi waheshimiwa kwa kukubali kugawanya kwa mbili mshahara wenu uliokuwa hauwafurahishe raia. Hiyo ni ishara ya uzalendo."

Kamerhe aahidi uwazi wa Bunge kwa umma

Kumekuwa na malalamiko ya wananchi kuhitaji kujua taarifa kadhaa kuhusu Bunge pamoja na Wabunge, hatua ambayo Spika Vital Kamerhe ameahidi ataimarisha uwazi katika kila kitu na yeyote atakayetaka kuelewa ukweli kuhusu usimamizi wa bunge basi ajielekeze bungeni ili kutoeneza uvumi usio na msingi.

Soma pia:DRC yatangaza baraza lake jipya la mawaziri la watu 54

"Sitakubali yeyote yule kuchafua sura ya taasisi kuu kama na hii. Nataka kila mtu kujuwa kwamba wabunge wanapokea mishahara yao kupitia benki. Munaweza kudhibitisha yote na hivyo kuacha kutengeneza uvumi."

Viongozi wawili wa upinzani DRC warejea Kinshasa

01:24

This browser does not support the video element.

Upande mwengine Spika Kamerhe alisisitiza kwamba kipindi hiki hakutakuwa na nyongeza ya mishahara ya wabunge.

Licha ya hatua hiyo ya Bunge, bado baadhi ya Wakongo wamekuwa na mashaka wakidhani wabunge watakuwa na fedha nyingine ambazo hazitawekwa wazi. Huku mwalimu na askari wakiendelea kupokea mishahara isiyo ya kuridhisha hata kidogo.

 

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW