1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kongo na M23 wasaini mfumo wa kusimamia usitishwaji mapigano

14 Oktoba 2025

Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo na waasi wa M23 wanaoungwa mkono na Rwanda leo wametia saini makubaliano ya kuanzisha mpango wa kufuatilia usitishwaji wa mapigano huko Doha.

Wawakilishi wa serikali ya Kongo na wanamgambo wa M23 huko Doha
Wawakilishi wa serikali ya Kongo na wanamgambo wa M23 huko DohaPicha: Karim Jaafar/AFP

Haya yamesemwa katika taarifa na wizara ya mambo ya kigeni ya mpatanishi wa pande hizo mbili, Qatar.

Taarifa hiyo imeongeza kuwa Qatar, Marekani na Umoja wa Afrikawatashiriki katika mpango huo kama waangalizi tu.

Doha imesema kuwa mpango huo utasimamia utekelezwaji wa usitishwajiwa kudumu wa mapigano, utachunguza na kuthibitisha ripoti za ukiukwaji na kufanya mawasiliano na pande husika kwa ajili ya kuzuia kurudiwa kwa uhasama.

Makubaliano haya ya leo yanafuatia makubaliano ya usitishwaji mapigano ya awali yaliyotiwa saini na pande zote mbili huko huko Doha mnamo mwezi Julai.

Wanamgambo wa M23 walikuwa wanasisitiza kutafuta makubaliano yao wenyewe ya amani na Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo wakidai makubaliano ya DRC na Rwanda yaliyotiwa saini Juni yaliacha masuala ambayo bado yanastahili kuangaziwa.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW