1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kongo na Rwanda kutia saini makubaliano ya amani

25 Aprili 2025

Kongo na Rwanda, leo zinapanga kusaini makubaliano ya kukuza amani na maendeleo ya kiuchumi mjini Washington, kama sehemu ya msukumo wa kidiplomasisa wa kusitisha ghasia.

Rais wa Rwanda Paul Kagame ( kushoto)  Kiongozi wa Qatar Sheikh Tamim
bin Hamad Al-Thani (katikati) na Rais wa Kongo Felix Tshisekedi (kulia) katika mkutano mjini Doha mnamo Machi 18, 2025
Rais wa Rwanda Paul Kagame ( kushoto) Kiongozi wa Qatar Sheikh Tamim bin Hamad Al-Thani (katikati) na Rais wa Kongo Felix Tshisekedi (kulia)Picha: MOFA QATAR/AFP

Makubaliano yanayotarajiwa kutiwa saini kati ya Kongo na Rwanda  katika hafla na waziri wa mambo ya nje wa Marekani Marco Rubio, yanakuja katika wakati ambapo Marekani iko kwenye mazungumzo ya kuwekeza mabilioni ya dola nchini Kongo yenye utajiri wa madini.

Kagame akubali rai ya Marekani kukomesha mapigano Kongo

Wiki hii, Rwanda imesema pia inazungumza na Marekani kuhusu uwezekano wa mkataba wa madini.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW