MigogoroJamhuri ya Kidemokrasia ya Congo
Kongo na Rwanda kuja na rasimu ya makubaliano ya amani
26 Aprili 2025
Matangazo
Haya ni kulingana na makubaliano yaliyotiwa saini na mataifa hayo mawili jana mjini Washington, Marekani, kama sehemu ya juhudi za kidiplomasia za kumaliza ghasia huko mashariki mwa Kongo.
Hatua hiyo inaibua matumaini kwamba mapigano yaliyoshuhudiwa hivi karibuni katika mzozo uliodumu kwa miongo kadhaa huenda yakapungua, licha ya miito ya kusitisha mapigano kutozaa matunda.
Pande zote mbili aidha zimekubaliana kushirikiana katika uratibu wa kukabiliana na makundi yenye silaha na mitandao ya uhalifu.
Makubaliano hayo yaliyofikiwa katikati ya hatua kubwa zilizopigwa na waasi wa M23, yanatarajiwa pia kufungua milango ya uwekezaji mkubwa wa Marekani kwenye ukanda huo wenye hifadhi kubwa ya madini ikiwa ni pamoja na dhahabu.