Kongo na Rwanda zasisitiza haja ya kuheshimu usitishaji vita
6 Novemba 2024Waakilishi wa Kongo na Rwanda walikutana na waziri wa mambo ya nje wa Angola Tete Antonio mjini Goma katika jimbo la Kivu Kaskazini, mashariki mwa Kongo, karibu na mpaka kati ya Kongo na Rwanda kuzindua kamati ya kufuatilia ukiukaji wa makubaliano ya kusitishwa kwa vita.
Angola kuongoza juhudi za upatanishi kati ya Rwanda na DRC
Baada ya mkutano huo, Antonio aliwaambia waandishi wa habari kwamba wote walisisitiza kuhusu haja ya kuheshimu makubaliano hayo na kuongeza kuwa njia ya sawa ni kupatikana kwa amani.
Rwanda yasema bado iko katika mchakato wa kutafuta amani
Kwa upande wake, waziri wa mambo ya nje wa Kongo Therese Kayikwamba Wagner, hakutoa tamko lolote baada ya mkutano huo.
Waziri wa mambo ya nje wa Rwanda Olivier Nduhungirehe, alisema nchi yake bado iko katika mchakato wa kutafutaamani.
Kamati hiyo ya kufuatilia usitisahji wa mapigano itaongozwa na Angola na kujumuisha waakilishi wa Kongo na Rwanda.