1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kongo: Vijana wajadili mchango wao katika ujenzi wa amani

Mitima Delachance12 Agosti 2024

Vijana nchini Kongo vijana wamekutana mjini Bukavu katika hafla kubwa ya fikra kuhusu mchango wa vijana katika ujenzi wa amani na maendeleo ya kudumu.

Maandamano ya vijana Kongo
Picha: Aubin Mukoni/AFP/Getty Images

Hafla hii iliwaleta pamoja vijana tofauti kutoka mashirika ya vijana themanini na saba kutoka pembe mbalimbali za jimbo la Kivu Kusini waliojadili masuala ya amani, maendeleo na ujasiriamali wa vijana, hasa wakati huu ambapo maeneo mengi ya mashariki mwa Kongo yanakabiliwa na changamoto za kiusalama za kila mara. Eric Baganda ni mratibu wa vijana Wakatoliki katika Jimbo la Kivu Kusini. Anasema lengo kuu ni kuwahamasisha vijana kurejea katika uzalendo.

Soma pia: DRC: Raia wataka ghasia kusitishwa Kivu Kaskazini na Ituri

Radio, chombo cha kueneza amani Kongo

04:11

This browser does not support the video element.

Vijana wa Kongo pia walitumia fursa hii kuchambua matatizo yanayowasukuma kuingia kwenye ukosefu wa maadili. Walibainisha kuwa ukosefu wa ajira umewaingiza wengi wao kwenye vitendo vilivyo kinyume na sheria. Hata hivyo, wanahisi kwamba inawezekana kubadili mambo vyema. Joella Sambo ni Msimamizi wa Baraza la Vijana wa Kivu Kusini, anatoa ujumbe wa amani na mshikamano na kuwahimiza vijana kufanya ujasiriamali:

 Papa Francis awarai vijana wa Kongo kupiga vita rushwa

Katika hafla hii, waziri husika na vijana wa Kivu Kusini Catherine Balemba alisifu kile anachokiita kuwa maendeleo makubwa katika namna ambavyo serikali ya Kongo inajali usimamizi wa vijana wakati huu na anaahidi kuimarisha zaidi ushirikiano kati ya mamlaka na vijana:

Wakati wa hafla hiyo, takwimu mbalimbali zilizochapishwa na miungano ya vijana zimeonesha kwamba vijana wenye umri wa chini ya miaka 25 wanawakilisha asilimia sitini na nane ya wakazi wa Kongo. Vijana wanatumai kwamba uwezekano na fursa zinazotolewa kwao pia zitaamua mustakabali wa nchi ya Kongo yenye utajiri wa mali na rasilimali.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW