Kongo yafungwa 2-1 na Chile mchezo kuelekea Kombe la Dunia
10 Juni 2026
Matangazo
Timu hiyo, The Leopards, ambayo maandalizi yake kuelekea Kombe la Dunia yaliingia kiwingu kutokana na mlipuko wa ugonjwa wa Ebola nchini Kongo, ilicheza mechi hiyo bila kuwepo mashabiki kwenye mji wa Orleans nchini Ufaransa.
Hapo kabla mechi hiyo ilikuwa ichezwe kusini mwa Uhispania, lakini meya wa mji mchezo huo ulikopangwa alikataa kutoa kibali kwa wasiwasi wa virusi vya Ebola licha ya kikosi cha Kongo kupiga kambi barani Ulaya hata kabla ya mlipuko wa sasa.
Kongo inarejea kucheza Kombe la Dunia kwa mara ya kwanza tangu mwaka 1974 na imepangwa kundi K ikiwa pamoja na Ureno, Colombia na Uzbekistan.