1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kongo yaomba msaada wa dola bilioni 2.25 za msaada wa kiutu

23 Februari 2023

Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo na shirika la misaada ya kibinadamu la Umoja wa Mataifa zimeomba msaada wa dola bilioni 2.25 mwaka huu kwa nchi hiyo maskini na iliyokumbwa na vita upande wa mashariki.

Katika taarifa yake iliyotolewa jana, Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Kuratibu Masuala ya Kibinadamu (OCHA), ilisema fedha hizo zitakidhi mahitaji muhimu ya watu milioni 10, katika nchi hiyo yenye takriban milioni 100.

Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo ndiyo mmoja ya mataifa maskini zaidi duniani, licha ya kuwa na hifadhi kubwa ya shaba, cobalt na madini mengine. Zaidi ya watu milioni 26 nchini humo wanakumbwa na hali ya ukosefu wa chakula kulinga na OCHA, huku mzozo ukiwa umewakosesha makazi watu milioni 5.7, idadi kubwa zaidi barani Afrika.