1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kongo yaripoti visa vipya 1,000 vya Mpox

21 Agosti 2024

Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo imeripoti zaidi ya visa vipya 1,000 vya homa ya Mpox katika wiki iliyopita hadi kufikia jana.

Mama wa Kikongo akimchunguza mtoto wake kama ana Mpox
Mama anaeishi kambini huko Goma akimchunguza mwanawe kama kapata maambukizi ya Mpox Julai 18, 2024.Picha: Arlette Bashizi/REUTERS

Visa hivyo vipya vimeripotiwa wakati ambapo maafisa wa afya barani Afrika wakiomba chanjo zinazohitajika kusaidia kupambana na kitisho kinachoongezeka cha ugonjwa hupo katika barani Afrika.Huku visa vya Mpox vikiripotiwa katika nchi 12 kati ya 54 za Afrika wakati wa miripuko ya ugonjwa huo, Kongo imerekodi visa vingi zaidi mwaka huu. Kituo cha Kuzuia na Kudhibiti Magonjwa barani Afrika, CDC, kimeeleza kuwa kati ya jumla ya visa 18,910 kwa mwaka huu wa 2024,asilimia 94 au visa 17,794 vimerekodiwa nchini Kongo. Mkurugenzi mkuu wa CDC, Jean Kaseya amesema nchi nyingi za Afrika zilizoathirika zina uwezo mdogo wa kupima na kufuatilia.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW