Kongo yataka msemaji wa MONUSCO kufukuzwa nchini humo
3 Agosti 2022Matangazo
Hii ni kutokana na kauli aliyoitoa, iliyotajwa kuwa yenye madhara yasiyofutika na yasiyo sahihi.
Hayo yanajiri wakati Kinshasa ikitangaza kutatathmini upya mpango wa kuwaondoa askari wa MONUSCO kufuatia maandamano ya vurugu wiki iliyopita, na kuashiria uwezekano wa kuwalazimisha wafanyakazi wa ujumbe huo kuondoka mapema kuliko ilivyotarajiwa.
Kupitia taarifa, serikali iliagiza hapo jana kufanyika mkutano na MONUSCO ili kujadili mpango wake wa kuondoka nchini humo. Kongo imesema raia 29 na wanajeshi wanne wa MONUSCO waliuawa wakati wa maandamano yaliyotokea mashariki mwa nchi hiyo.
Waandamanaji walikuwa wanashinikiza askari hao kuondoka kwa kushindwa kuwalinda raia dhidi ya mashambulizi ya makundi ya waasi.