Kongo yatangaza mripuko wa homa ya nyani
24 Aprili 2024Matangazo
Waziri wa Afya wa nchi hiyo, Gilbert Mokoki amesema hakuna vifo vilivyorekodiwa kufikia sasa, lakini ametoa wito kwa umma kuchukua tahadhari, kwa kukaa mbali na wanaoshukiwa kuambukizwa homa hiyo, kuepuka kukaribiana na wanyama na kutoshika nyama za wanyamapori kwa mikono mitupu.
Jamhuri ya Kongo yaripoti visa kadhaa vya homa ya nyani, mpox
Kulingana na Shirika la Afya Duniani (WHO) homa ya nyani iligunduliwa kwa mara ya kwanza kwa binaadamu katika nchi jirani ya Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo mwaka 1970.
Dalili zake zikiwa ni pamoja na homa, maumivu na vidonda kwenye ngozi.