1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kongo yatinga Kombe la Dunia baada ya miaka 52

1 Aprili 2026

Bao lililofungwa katika dakika ya 100 ya mechi na beki wa klabu ya nchini England, Burnley, Axel Tuanzebe, limeipelekea Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo kufuzu kwenye mashindano ya Kombe la Dunia.

Fußball-WM 2026 | Playoff-Finale | DR Kongo vs. Jamaika | Kongos Spieler feiern den Sieg
Kongo yatinga Kombe la Dunia baada ya miaka 52Picha: Eduardo Verdugo/AP Photo/picture alliance

Mashindano hayo yatafanyika huko Marekani, Canada na Mexico kuanzia mwezi Juni.

Kongo wamepata fursa hiyo ya kuwa mwakilishi wa 10 wa Afrika kwenye mashindano hayo baada ya kuilaza Jamaica 1-0 katika mechi ya fainali ya mchujo.

Hii ndiyo mara ya kwanza Kongo kufuzu kwenye mashindano hayo katika kipindi cha miaka 52 kwani mara ya mwisho kufuzu ilikuwa 1974 ambapo nchi hiyo ilikuwa inafahamika kama Zaire.

Wako kwenye kundi moja na Ureno, Colombia na Uzbekistan. Irak ndiyo timu iliyofuzu ya mwisho kabisa jana baada ya kuifunga Bolivia 2-1 na Italia nayo haitoshiriki mashindano hayo baada ya kufungwa na Bosnia Herzegovina 4-1 kupitia mikwaju ya penalti baada ya mechi kuishia sare 1-1.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW