Kongo yatumaini kupata suluhisho ya mchuano dhidi ya Chile
3 Juni 2026
Matangazo
Timu hiyo ya Kongo ilikuwa imepangwa kucheza dhidi ya Chile tarehe 9 Juni katika mji wa La Línea de la Concepción, lakini meya wa eneo hilo Juan Franco alizuia mechi hiyo kufanyika kutokana na wasiwasi wa kiafya.
Franco ameiambia redio Cope ya Uhispania kwamba wataalamu wa eneo hilo na wale wa jimbo la Andalusia walisema nyaraka zilizowasilishwa na ujumbe wa Congo zilionekana kutoridhisha na wakachagua ''njia ya tahadhari ya kiwango cha juu zaidi.”
Shirikisho la Soka la Congo (FA) limesema kuwa hatua zote muhimu zilichukuliwa ili kutimiza masharti yote ya kiafya na kimichezo, na kwamba "linazingatia kikamilifu taratibu za kimataifa.”