1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kongo yawaachia wafungwa 600 ili kupunguza msongamano

Sylvia Mwehozi
22 Septemba 2024

Mamlaka nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo zimewaachia huru wafungwa 600 kutoka gereza kuu la nchi, kama sehemu ya mchakato unaolenga kupunguza msongamano ndani ya magereza.

DR Kongo | Wanajeshi wakiwa wamedhibiti jaribio la kutoroka katika Gereza la Makala mjini Kinshasa
Wanajeshi wakiwa wamedhibiti jaribio la kutoroka katika Gereza la Makala mjini KinshasaPicha: Hardy Bope/AFP

Mamlaka nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo zimewaachia huru wafungwa 600 kutoka gereza kuu la nchi, kama sehemu ya mchakato unaolenga kupunguza msongamano ndani ya magereza. Waziri wa sheria Constant Mutamba alitangaza hatua hiyo wakati wa hafla katika Gereza kuu la Makala katika mji mkuu wa Kongo, Kinshasha. Mutamba amesema serikali ina mipango ya kujenga gereza jipya mjini Kinshasa, bila kutoa maelezo zaidi.Wafungwa watoroka gerezani DRC

Kulingana na ripoti ya hivi karibuni ya shirika la kimataifa la Amnesty International, gereza la Makala ambalo ndio kubwa zaidi nchini humo lina uwezo wa kuchukua wafungwa 1,500, lakini linawahifadhi zaidi ya wafungwa 12,000, wengi wao wakisubiri kesi. Mapema mwezi huu, kulitokea jaribio la kuvunja gereza ambapo watu 129 walikufa, wakiwemo wale waliopigwa risasi na walinzi na wengine kufariki katika mkanyagano.