1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kongo yawanyonga watu102, wengine 70 wangojea hukumu yao

6 Januari 2025

Wizara ya sheria ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo imesema watu 102 wamenyongwa na wengine 70 wamepangiwa kupewa adhabu hiyo.

DR Kongo | Ausbruchsversuch aus dem Makala Gefängnis in Kinshasa
Vikosi vya usalama vya serikali nje ya gereza la Makala huko Kinshasa, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Septemba 2, 2024.Picha: AP Photo/picture alliance

Kwa mujibu wa taarifa ya wizara hiyo iliyotolewa jana, watu hao, wanaume wenye umri wa baina ya miaka 18 na 35, walikuwa majambazi wenye silaha, wanaofahamika kama Kuluna, na walinyongwa kwenye gereza la Angenga kaskazini magharibi mwa nchi hiyo.  Arubaini na tano walinyongwa mwishoni mwa mwezi Disemba na wengine 57 walinyongwa ndani ya masaa 48 yaliyopita. Shirika la habari la AP limeripoti kuwasili kwa ndege iliyobeba watu wengine 70 kwenye mji wa Angenga, ingawa serikali haijasema chochote kuhusu wafungwa hao. Wizara ya sheria imesema kundi la tatu la wafungwa hao watanyongwa kama makundi mawili ya mwanzo. Hukumu ya kifo ilikuwa imefutwa tangu mwaka 1981, lakini ikarejeshwa tena mwaka 2006, lakini utekelezaji wake 2003.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW