Korea kaskazini na China zakubaliana kulinda maslahi yao
27 Januari 2024Siku ya Ijumaa, China imesema kuwa imekubaliana na Korea Kaskazini kuimarisha mawasiliano ya kimkakati "katika ngazi zote" na kuthibitisha tena kuweko kwa msimamo usioyumba juu ya kuimarisha uhusiano huo wakati Sun alipokutana na mwenzake wa Korea Kaskazini, Pak Myong Ho, mjini Pyongyang.
Soma pia:China yataka mdahalo na Korea Kaskazini
Mkutano huo ni hatua ya hivi karibuni ya ushirikiano wa Korea Kaskazini na China pamoja na Urusi wakati ikiimarisha makabiliano yake na Marekani na Korea Kusini.
Soma pia:Xi ahimiza utatuzi wa amani wa suala la Korea Kaskazini
Korea Kaskazini imeimarisha kwa kiasi kikubwa uhusiano wake na mataifa hayo mawili ambayo ni wanachama wa kudumu wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa na washirika wa jadi, ambayo yamesimama na nchi hiyo inapozidisha kasi yake ya utengenezaji wa silaha za kimkakati.