1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUrusi

Korea Kaskazini yaahidi kuunga mkono uvamizi Ukraine

12 Juni 2023

Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un ameahidi kuunga mkono kikamilifu uvamizi wa Urusi nchini Ukraine katika ujumbe aliyoutoa kwa Rais Vladimir Putin wakati Moscow ikiadhimisha siku ya kitaifa.

75. Gründungstag seiner Streitkräfte in Nordkorea
Picha: KCNA VIA KNS/AFP

Kim alinukuliwa na shirika la habari la Korea Kaskazini KCNA kuwa kwa hakika haki itashinda na watu wa Urusi wataendelea kuongeza utukufu katika historia ya ushindi, na kuongeza kuwa urafiki kati ya Korea Kaskazini na Urusi ni muhimu kimkakati na umekuwepo kwa karne nyingi.

Mara tu baada ya uvamizi wa Urusi kuanza mwezi Februari mwaka jana, Ukraine ilivunja mara moja uhusiano wa kidiplomasia na Korea Kaskazini.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW