Korea Kaskazini yafanya jaribio la ndege isiyokuwa na rubani
24 Machi 2023Shirika la habari la nchi hiyo, KCNA, limeripoti hayo hii leo, Ijumaa, wakati kiongozi wa nchi hiyo, Kim Jong Un, akitowa onyo kwamba luteka za kijeshi zinazofanywa kwa pamoja na Korea Kusini na Marekani zinapaswa kusitishwa.
Katika jaribio hilo la Korea Kaskazini ndege hiyo ilisafiri kwa kima cha futi 260 mpaka 500 chini ya maji kwa muda wa saa 59 na kuripua mabomu yasiyokuwa na nguvu za nyuklia chini ya bahari kwenye pwani ya mashariki mwa nchi hiyo hapo jana Alhamisi.
Soma pia: Kim aamuru uimarishwaji wa mazoezi ya kijeshi
Wachambuzi wanasema nchi hiyo inazionesha Marekani na Korea Kusini, uwezo wake uliozidi kutanuka wa nguvu za nyuklia, ingawa wachambuzi pia wana mashaka ikiwa chombo hicho cha kusafiri chini ya maji kiko tayari kwa matumizi.