1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Migogoro

Korea Kaskazini yafanya jaribio la kombora la Balistiki

4 Januari 2026

Korea Kaskazini imefyatua makombora kadhaa ya balistiki kutoka pwani yake ya mashariki leo Jumapili, kwa mujibu wa jeshi la Korea Kusini.

Pyongyang 2026 | Kim Jong-na binti yake Kim Ju-ae katika sherehe za mwaka mpya
Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-na binti yake Kim Ju-ae katika sherehe za mwaka mpyaPicha: KCNA/REUTERS

Korea Kaskazini imefyatua makombora kadhaa ya balistiki kutoka pwani yake ya mashariki leo Jumapili, kwa mujibu wa jeshi la Korea Kusini. Hayo yanajiri siku moja baada ya operesheni kubwa ya kijeshi ya Marekani dhidi ya mshirika wa kisoshalisti wa Pyongyang, Venezuela.

Ufyatuaji huo wa kwanza kwa mwaka huu ulifanyika saa chache kabla ya kiongozi wa Korea Kusini kuelekea China kwa mkutano wa kilele unaotarajiwa kujadili uhusiano na Korea Kaskazini.

Wizara ya ulinzi ya Seoul ilisema imegundua vilipuzi kadhaa, vinavyodhaniwa kuwa makombora ya balistiki vilivyofyatuliwa karibu na mji mkuu wa Korea Kaskazini, Pyongyang.

Mara ya mwisho kwa Pyongyang kufyatua kombora la balestiki ilikuwa mwezi Novemba, baada ya Rais wa Marekani Donald Trump kuidhinisha mpango wa Korea Kusini wa kujenga manowari inayotumia nyuklia.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW