Korea kaskazini yafanya jaribio ya makombora ya uwezo mdogo
31 Mei 2008Matangazo
PYONG YANG
Korea Kaskazini imefahamisha kwamba imefanya majaribio ya makombora yake matatu yasiyokuwa na uwezo wa kufika mbali katika pwani yake ya magharibi.Kwa mujibu wa shirika la habari la Korea Kusini la Yonhap duru za serikali ya Korea Kaskazini zimesema hatua hiyo ni sehemu mojawapo ya mazoezi ya kijeshi yanayohusisha majaribio ya makombora yaliyotengenezwa Urussi yenye uwezo wa kufika kilomita 46.
Taarifa hiyo imekuja baada ya wajumbe kutoka korea hizo mbili Kusini na Kaskazini kukutana mjini Beijing hapo jana kwa muda wa kiasi cha saa moja katika juhudi za kukomesha mpango wa kinuklia wa Korea Kaskazini.