Korea Kaskazini yafanya majaribio mengine ya makombora
22 Julai 2023Hayo yameripotiwa na shirika la habari la Korea Kusini, Yonhap likinukuu maafisa wa jeshi la nchi hiyo. Ufyetuaji huo umefanyika ikiwa zimepita siku tatu pekee tangu nchi hiyo ilipofanya majaribio mengine ya makombora mawili ya masafa marefu wakati mivutano inaongezeka kwenye eneo la rasi ya korea.
Soma zaidi: Marekani, Japan na Korea Kusini zalaani hatua ya Korea Kaskazini kurusha kombora
Wakati hayo yakijiri kundi la mataifa tajiri la G7 na nchi nyingine tatu zimeandika barua kwenda kwa China ya kuitaka nchi hiyo isaidie kuizuia Korea Kaskazini kuepuka vikwazo vya Umoja wa Mataifa kwa kutumia eneo la bahari la China.
Kundi hilo la mataifa ya G7 na washirika wengine limesema lina mashaka juu ya uwepo kwa meli za mafuta kwenye eneo la bahari la China la Sansha Bay ambazo inaamini zinafanya biashara ya mafuta na Korea Kaskazinina kukwepa vikwazo ilivyoewekewa nchi hiyo na Umoja wa Mataifa.