1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Korea Kaskazini yafanya majaribio ya Droni za kulipuka

Sylvia Mwehozi
15 Novemba 2024

Vyombo vya habari vya umma nchini Korea Kaskazini vimeripoti mapema leo kwamba nchi hiyo imefanya majaribio ya ndege zisizo na rubani zenye uwezo wa kulipuka na kulenga shabaha.

Kim Jong Un akikagua uzalishaji wa droni
Kim Jong Un akikagua uzalishaji wa droni Picha: KCNA VIA KNS/AFP

Vyombo vya habari vya umma nchini Korea Kaskazini vimeripoti mapema leo kwamba nchi hiyo imefanya majaribio ya ndege zisizo na rubani zenye uwezo wa kulipuka na kulenga shabaha, wakati kiongozi wa nchi hiyo Kim Jong Un akihimiza uzalishaji wa silaha hizo kwa wingi.Korea Kaskazini yajiandaa kufanya jaribio la nyuklia

Kwa mujibu wa shirika la habari la Korea Kaskazini KCNA, Kim ameonyesha kuridhishwa na mchakato wa kutengeneza silaha akibainisha jinsi ndege za Droni zinavyozidi kuwa na umuhimu katika vita vya kisasa.

Majaribio hayo ya hivi karibuni yanafanyika wakati Marekani, Korea Kusini na Japan zikifanya luteka za pamoja za kijeshi zinazojumuisha ndege za kivita za hali ya juu.

Aidha pia manowari ya Marekani imeripotiwa kuwa ilikuwa imepiga kambi karibu na mipaka ya kimataifa kama ishara ya ulinzi wa mataifa hayo dhidi ya Pyongyang.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW