SiasaKorea Kusini
Korea Kaskazini yafanya mkutano wa usalama wa kitaifa
15 Oktoba 2024Matangazo
Mkutano huo mjini Pyongyang ulihudhuriwa na maafisa wakuu wa usalama wa nchi hiyo akiwemo mkuu wa jeshi na maafisa wengine wa kijeshi pamoja na mawaziri wa usalama wa nchi na ulinzi.
Shirika la habari la KCNA limeripoti kuwa Kim alitoa mwelekeo wa hatua za haraka za kijeshi na kuelekeza kuhusu majukumu ya kutimizwa katika operesheni ya kuzuia vita na kile alichokiita utumiaji wa haki ya kujilinda.
Soma pia: Korea kaskazini iko tayari kuishambulia Korea Kusini
Mkutano huo unakuja huku Korea Kaskazini yenye silaha za nyuklia ikiishutumu Kusini kwa kurusha droni juu ya mji wake mkuu na kupeleka wanajeshi kwenye mpaka wake, huku Korea Kusini ikisema jana Jumatatu kuwa iko "tayari kabisa" kujibu ikiwa itashambuliwa.