Korea Kaskazini yafunga balozi zake nyingi Barani Afrika
1 Novemba 2023Korea Kaskazini inatarajiwa kufunga balozi zake nyingi ikiwemo Uhispania, Hong Kong na katika mataifa mengi ya Afrika. Hatua hii huenda ikaathiri asilimia 25 ya balozi za taifa hilo duniani.
Wizara ya muungano wa Korea Kusini imesema hatua ya jirani yake inaonesha wazi kuwa imelemewa kifedha kufuatia vikwazo vya kimataifa ilivyowekewa.
Soma pia kuhusu: Korea Kusini, Marekani na Japan wailaani Korea Kaskazini
Kwa mujibu wa shirika la habari la Korea Kaskazini, siku ya Jumatatu balozi wa taifa hilo alifanya ziara ya mwisho kwa viongozi wa Angola na Uganda wiki iliyopita huku vyombo vya ndani vya habari vya mataifa hayo vikiripoti kufungwa kwa balozi hizo.
Uganda na Angola zimekuwa na ushirikiano wa kirafiki na Korea Kaskazini tangu mwaka 1970 hasa katika ushirikiano wa kijeshi na kushiriki ujenzi wa miradi tofauti ya miundo mbinu.