SiasaKorea Kaskazini
Korea Kaskazini yafyatua makombora ya masafa mafupi
23 Desemba 2022Matangazo
Makombora hayo yametumwa siku chache baada ya ndege za kivita za Marekani na Korea Kusini kufanya luteka ya pamoja katika hatua ambayo Korea Kaskazini inaiona kama mazoezi ya uvamizi.
Jeshi la Korea Kusini limegundua ufyatuaji huo wa makombora majira ya saa kumi na nusu jioni kwa saa za Asia Mashariki.
Siku ya Jumanne, ndege za kivita zenye uwezo wa kuwa na nyuklia za Marekani ziliruka katika Rasi ya Korea katika luteka ya pamoja na ndege za kivita za Korea Kusini.
Wizara ya Ulinzi ya Korea Kusini imesema luteka hiyo ilikuwa sehemu ya makubaliano ya pande hizo mbili katika kuimarisha dhamira ya Marekani ya kumlinda mshirika wake wa Asia kwa uwezekano wowote wa kijeshi, ikiwemo nyuklia.