SiasaAsia
Korea Kaskazini yafyetua makombora 10 kuelekea baharini
14 Machi 2026
Matangazo
Hayo yameelezwa na jeshi la Korea Kusini na kuongeza kuwa makombora hayo yalirushwa kutoka eneo la Sunan, uliopo uwanja wa ndege wa kimataifa wa Pyongyang , na kusafiri umbali wa kilomita takriban 350.
Jeshi la Seoul limeimarisha ulinzi na kujiweka tayari dhidi ya uwezekano wa mashambulizi zaidi huku ikibadilishana taarifa na Marekani pamoja na Japan.
Wakati huo huo, waziri wa Ulinzi wa Japan Shinjiro Koizumi, amesema makombora hayo yalitua nje ya kitovu cha kipekee cha uchumi katika bahari ya Japan lakini hakukuwa na ripoti za uharibifu wa ndege au meli.
Mashambulizi hayo yanakuja huku utawala wa rais wa Marekani Donald Trump ukiendesha vita vinavyozidi kuongezeka katika eneo la Mashariki ya Kati.